3347; Kama hata mpumbavu anaweza kufanya.

Kutoka mezani kwa Kocha,

Rafiki yangu mpendwa,
Huwa ni rahisi kuhukumu matokeo tunayopata, lakini tunasahau juhudi ambazo tumeweka.
Kwa sababu matokeo hayaji kama ajali, bali yanatokana na juhudi zinazowekwa.

Charlie Munger alikuwa na msingi wake binafsi kwamba badala ya kutaka kuonekana ana akili sana, alikuwa anakazana asiwe mpumbavu.
Kwa kuepuka upumbavu, aliepuka mengi yasiyo sahihi na hatimaye kuonekana kama mwenye akili sana.

Hilo ni muhimu kujifunza na kufanyia kazi, kuepuka upumbavu.
Na njia bora ya kufanya hivyo ni kujiuliza nani anaweza kufanya kile unachotaka kufanya.
Kama hata mpumbavu anaweza kufanya kile unachotaka kufanya, basi hupaswi kukifanya.
Kwa sababu ukikifanya, utaishia kupata matokeo wanayoyapata wapumbavu.

Ukifanya kile ambacho hata mpumbavu anaweza kufanya, unakuwa umechagua matokeo wanayopata wapumbavu. Hivyo usije ukashangaa pale matokeo yanapokuja kwa namna hiyo.

Usihangaike sana na namna gani ya kuwaonyesha wengine jinsi ulivyo na akili ngi vj
Kazana na kuepuka upumbavu, kwa kutokufanya yale ambayo wapumbavu wanafanya na utaweza kuzalisha matokeo bora sana.

Kwenye jamii ya KISIMA CHA MAARIFA, ambayo ni jamii ya tofauti tunayoijenga, tunaepuka sana upumbavu kama ukoma.
Haturudii kufanya yale yale yaliyozoeleka kufanywa, bali tunapata MAARIFA sahihi na kuyaweka kwenye VITENDO kwa kuchukua hatua sahihi na hayo yanapelekea kupata matokeo ya tofauti ambayo ndiyo MAFANIKIO.

Kwa kukaa kwenye huo msingi mkuu, tunaepuka upumbavu mwingi ambao ungetukwamisha kwenye yale tunayoyataka.

Kama hata mpumbavu anaweza kufanya kitu, kataa kabisa kukifanya. Maana utakachofanya ni kuonyesha na wewe ni mpumbavu.
Epuka kabisa yote yanayohusiana na upumbavu na utajiepusha na changamoto nyingi zinazoweza kukukwamisha.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe