Rafiki yangu mpendwa,
Mtu aliyeishi hapa duniani na kufariki kabla ya mwaka 1950, alidhani miaka 50 baadaye, yaani kuanzia mwaka 2000 na kuendelea, maisha ya watu duniani yatakuwa bora sana.
Hiyo ni kwa sababu ya maendeleo makubwa ya teknolojia ambayo yalikuwa yanatokea kwa kasi kubwa. Ukweli ni maendeleo ya teknolojia yamekuwa yanatokea kwa kasi kubwa. Lakini sasa, cha kushangaza, maisha ya watu wengi bado siyo bora kama ilivyodhaniwa.

Mfano, mchumi mmoja maarufu aliwahi kutabiri kwamba miaka ya mbele, watu wasingehitajika kuwa wanafanya kazi masaa mengi, kwa sababu teknolojia zinarahisisha sana kazi. Kweli, teknolojia zimerahisisha kazi, lakini muda wa watu kufanya kazi umeongezeka kuliko kupungua. Yaani watu wanafanya kazi masaa mengi zaidi kuliko ilivyotegemewa.
Ni dhahiri ubora wa maisha kwa ujumla umeendelea kuimarika, kwa sasa watu wanaishi miaka mingi kutokana na ubora wa huduma za afya. Lakini pia idadi ya watu wanaoishi kwenye umasikini wa kupindukia imepungua. Kwa hivyo kijumla, hatua kubwa zinapigwa.
Lakini inapokuja kwa mtu binafsi, mtu mmoja mmoja, wengi sana wanashindwa kupata mafanikio makubwa ambayo wangeweza kuyafikia. Licha ya mazingira kuwa rafiki kwa wengi kuweza kufanya makubwa zaidi, bado wengi wanashindwa.
Maendeleo ya teknolojia yameondoa vikwazo vingi vilivyokuwa vinawazuia wengi kufanya yale waliyoyataka. Kwa sasa mtu anaweza kujifunza chochote anachotaka kujifunza na kuweza kuwasiliana kwa urahisi na yeyote duniani. Kwa sasa mtu anaweza kuanzisha biashara bila ya kuwa na mtaji wala eneo la kufanya biashara, kwa kutumia tu simu ya mkononi na mtandao, mtu anaweza kujenga biashara ambayo ni kubwa sana.
Lakini licha ya urahisi huo mkubwa wa kufanikiwa, mafanikio yamekuwa magumu sana zama hizi kuliko hata kipindi cha nyuma ambapo vikwazo vilikuwa vingi.
Je nini kinapelekea hili? Nini kinawakwamisha watu kiasi hicho? Hiki ni kitendawili ambacho wamekuwa wanashindwa kukitegua. Na hilo limekuwa linazidi kuwa kikwazo kwa watu kufanikiwa kwa kadiri ya ambavyo wangeweza.
Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA nimeeleza sababu kubwa mbili zinazowazuia watu kupata mafanikio makubwa kwenye zama hizi. Hizi ni sababu ambazo zimekuwepo kwenye zama hizi, huko nyuma hazikuwepo na hivyo watu waliweza kufanikiwa kwa kiasi, licha ya vikwazo kuwa vingi. Kwa sasa vikwazo vimepungua, lakini watu hawafanikiwi kwa sababu hizo mbili.
Karibu usikilize kipindi hiki cha ONGEA NA KOCHA uzijue sababu hizo mbili na hatua za kuchukua ili usikwamishwe na hizo sababu kwenye lengo lako la kujenga mafanikio makubwa.
Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani,
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi
0678 977 007 / amakirita@gmail.com
MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.