Rafiki yangu mpendwa,

Yupo nabii mmoja ambaye unabii wake umekuwa unatimia kwa uhakika kwenye maisha yako.

Kila anachotabiri kuhusu wewe, ndiyo hicho hicho kimekuwa kinatokea bila kukosa.

Hapo ulipo sasa, ni kwa sababu ya unabii wake ambao aliufanya siku za nyuma.

Na pale utakapokuwa kesho, kutatokana na unabii wake wa leo.

Je usingetaka kukutana na huyu nabii leo ili kesho yako iwe vile unavyotaka?

Kwa sababu, hebu fikiri amekuwa anakutabiria bila ya wewe kujua, vipi kama ukajua na ukamwambia nini hasa unachotaka kwenye maisha yako, na yeye akakutabiria hicho hicho kisha ukakipata?

Rafiki, huoni hiyo ni nafasi ya kipekee sana, nafasi ya kuchagua maisha yako yaweje kwa kumwambia nabii mkuu na kisha yeye kusema neno na ikawa kwa uhakika?

Katika hali hiyo, unapaswa kuchukua hatua ya kukutana na huyu nabii mara moja. Unapaswa kuacha kila unachokifanya na kukutana na nabii huyu. Kwa sababu ina haja gani ya kuhangaika wakati kesho yako tayari imeshapangwa na nabii huyo?

Hatua ya wewe kuchukua sasa hivi ni kukutana na huyu nabii wa uhakika kwako, kumwambia nini hasa unachotaka kwenye maisha yako na kisha yeye kukutabiria hicho bila ya kusita.

Baada ya yeye kukutabiria kile unachotaka, kinachofuata ni wewe kupokea kulingana na unabii huo.

Rafiki, mjue sasa nabii wako wa uhakika na jinsi ya kumtumia kufanikiwa kwa kuangalia kipindi cha ONGEA NA KOCHA hapo chini. Nimekueleza kwa kina kuhusu nabii huyo na jinsi ya kunufaika naye. Fungua sasa kujifunza na kuchukua hatua ili kuyabadili maisha yako kuwa bora zaidi ya yalivyo sasa.

Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani,

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi

0678 977 007 / amakirita@gmail.com

www.amkamtanzania.com

MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.