3352; Sifuri, moja na zaidi.
Kutoka mezani kwa Kocha,
Rafiki yangu mpendwa,
Hakuna namba ngumu kwenye maisha kama sifuri.
Ni namba ambayo hakuna namna unaweza kuiboresha, kwa sababu ni kitu kisichokuwepo kabisa.
Kutoka sifuri kwenda moja ndiyo hatua ngumu zaidi kwenye maisha.
Hiyo ni kwa sababu unaanza kitu ambacho hakipo kabisa au hujawahi kukifanya na hivyo kinakuwa kigeni kwako.
Kutoka moja kwenda kwenye namba nyingine zaidi ni zoezi rahisi. Hiyo ni kwa sababu tayari una historia ya kufanya na kuweza.
Hivyo unaweza kurudia kile ambacho tayari kimeshaleta matokeo.
Kazi yako kubwa ni kutoka sifuri kwenda moja. Hapo ndipo unapuvunja ukomo ambao umekuwa unakuzuia mara zote.
Ukishaweza kufanya hata mara moja tu, unaweza kufanya mara nyingi zaidi, maana unarudia tu kile ambacho kimefanya kazi tayari.
Unachohitaji ni kufanya kwa ubora zaidi ili kuweza kuzalisha matokeo ya uhakika zaidi.
Kama umeweza kupata moja, unaweza kupata 10, 100, 1000 na kuendelea. Ni wewe kurudia kwa ubora yale yaliyozalisha matokeo.
Chochote ambacho unakipata sasa, ila kwa namba ndogo, unaweza kukipata kwa ukubwa zaidi kama ukifanya kwa ubora.
Kama kipato chako ni kidogo, unaweza kukiongeza kwa kufanya kwa ubora zaidi yale yanayokupa matokeo kidogo.
Kazi yako kubwa ni kuvunja na kuvuka namba sifuri ambayo ni kikwazo kuliko namba nyingine yoyote.
Ukishavuka hiyo, nyingine zinazofuata zinawezekana kwa uhakika.
Kwenye jamii ya KISIMA CHA MAARIFA, ambayo ni jamii ya tofauti tunayoijenga, kazi yetu kubwa ni kufuta namba sifuri kwenye kila eneo la maisha yetu.
Tunahakikisha tunaibomoa sifuri popote ilipo kwenye maisha yetu ili tuweze kupiga hatua kubwa zaidi.
Tunajua hatuwezi kuboresha sifuri, kwa sababu ni kitu ambacho hakipo.
Hivyo tunakazana kuondokana nayo ili kupata mahali sahihi pa kuanzia na kupiga hatua kubwa kadiri ya tunavyotaka.
Ni maeneo gani ya maisha yako bado yana sifuri? Weka mkakati wa kuzitokomeza.
Halafu mwenye maeneo yote ambayo una namba ndogo, weka juhudi kuzikuza zaidi.
Boresha kile ambacho ulitanya na kupata matokeo hayo madogo na utaweza kupata matokeo makubwa zaidi.
Huhitaji kuja na ubunifu mpya kila wakati, unahitaji kuboresha kile ambacho tayari kinafanya kazi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe