3354; Thamani unayoongeza.

Kutoka mezani kwa Kocha,

Rafiki yangu mpendwa,
Kila kitu unachojihusisha nacho, swali la kwanza na muhimu kujiuliza ni thamani gani unayoitoa.
Kwa sababu hiyo ndiyo itakayopima ni mafanikio kiasi gani ambayo unaweza kuyafikia kwenye maisha yako.

Iko hivi, watu hawakupi kile unachotaka kwa sababu unakitaka sana, au unastahili sana.
Bali wanakupa kile unachotaka, kama na wao watapata kile wanachotaka.

Hivyo badala ya kuangalia sana ni nini unakwenda kupata wewe, angalia ni nini wengine wanaenda kupata.
Watu wanapenda kupata, wape kwa wingi na wao watakuwa tayari kukupa wewe pia.

Kila unapokuwa umekwama kupata kile unachotaka, anza kwa kujiuliza kile ulichotoa kwanza. Angalia ukubwa wa thamani unayoitoa na upime kama kweli thamani hiyo inaweza kupelekea wewe upate unachotaka.

Kwenye jamii ya KISIMA CHA MAARIFA, ambayo ni jamii ya tofauti tunayoijenga, kuongeza thamani kwa wengine ni moja ya msingi yote muhimu.
Kwa kila jambo tunalofanya, swali la kwanza tunalojiuliza ni thamani gani tunayotoa kwa wengine.
Kwa ukuaji tunaoutaka, tunajiuliza ni thamani ipi tunaweza kuongeza zaidi na kuwafikia wengi zaidi?

Ndani ya jamii hii bora sana tunayoijenga, kila kitu tunakipima kwa thamani ambayo inapatikana kupitia hicho.
Kwa kuhangaika na thamani ndiyo kunafungua njia nyingi za kupata yale tunayotaka.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe