Rafiki yangu mpendwa,
Kitu chochote kile ambacho hakijawahi kufanyika, huwa kinachukuliwa kama hakiwezekani kabisa. Watu wataamini kwamba kitu hicho hakiwezekani. Na hata pale watakapojaribu, wakikutana na ugumu wanakuwa wamejidhihirishia kwamba haiwezekani.
Ni mpaka pale anapotokea mtu asiyejua kama kitu hakiwezekani, au anayejua lakini akapuuza, anafanya na inawezekana. Baada ya hapo watu wanakuwa hawawezi tena kutumia sababu ya kutowezekana. Hivyo wanakuwa hawana budi bali kufanya.

Kwa maana hiyo basi rafiki yangu, mambo mengi unayojiambia kwa sasa hayawezekani, yanawezekana kama utaachana na hizo fikra za kwamba hayawezekani.
Na kuna njia mbili za kuondokana na hizo fikra kwa uhakika na ukaweza kufanya makubwa bila ya shida yoyote.
Njia ya kwanza ni kwa kuwatafuta ambao wameshafanya na kwa kujua wengine wameshafanya na wewe utapata msukumo wa kufanya na ikawezekana kabisa.
Njia ya pili ni kwa kuamua kwamba wewe utakuwa mtu wa kwanza kufanya na kuweka historia. Utatumia njia hii kama umetafuta ambao wameshafanya na ukawakosa. Hivyo badala ya kukata tamaa kwamba haiwezekani, unaamua wewe uwe mfano kwa wengine kwamba inawezekana.
Kitu unachohitaji sana ili kitu chochote kiwezekane ni wewe kuchukua hatua kwenye kukifanya. Bila ya kuchukua hatua, kila kitu kitabaki kuwa hakiwezekani. Lakini unapochukua hatua, hata kama ni ndogo kiasi gani, zinakusogeza karibu na kuwezekana. Zinakufundisha njia za kuboresha na kuweza kuona namna inavyowezekana.
Rafiki, nikualike ujifunze zaidi jinsi ya kufanya chochote kiwezekane kwako, fungua kipindi cha ONGEA NA KOCHA hapo chini upate kujifunza hili na uwe usiyezuilika katika kuzipambania ndoto zako.
Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani,
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi
0678 977 007 / amakirita@gmail.com
MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.