Rafiki yangu mpendwa,
Maisha hayajawahi kuwa rahisi kwa mtu yeyote hapa duniani. Kila mtu unayepishana naye, ana mambo yake ambayo anapambana nayo kama ulivyo wewe.
Lakini licha ya kila mtu kuwa anapitia magumu na changamoto mbalimbali, bado mafanikio yamekuwa yanatofautiana kwa watu. Kuna watu ambao wameweza kujenga mafanikio makubwa licha ya magumu wanayopita. Na kuna watu ambao wameshindwa kabisa kufanikiwa na kubaki chini.
Ukiwaangalia wanaofanikiwa na wanaoshindwa, hawana tofauti kubwa sana kwa nje. Ila ndani yao kuna misukumo inayotofautiana na ambayo ndiyo inasababisha tofauti ya mafanikio wanayoyapata.
Wale wanaofanikiwa licha ya magumu wanayokuwa wanayapitia kuna swali moja huwa wanajiuliza. Majibu ya swali hilo huwa yanawapa msukumo wa kufanya vitu vya tofauti na walivyokuwa wanavifanya awali.

Swali hilo linawafanya waione dunia kwa namna ya tofauti kabisa. Wanakuwa kama watu ambao walikuwa wamevaa miwani ya giza na kisha kuivua, kitu kinachowafanya waione dunia kwa umakini zaidi.
Majibu ya swali hilo muhimu ambalo na wewe unakwenda kujifunza hapa yanawaamsha sana kiasi cha wao wenyewe kuona ni wapi wamekuwa wanajikwamisha kwa muda mrefu. Na hilo linawafungulia milango ya mafanikio makubwa ambayo wanayapata kwa uhakika.
Wale wanaoshindwa na kubaki pale walipo huwa ni watu wa kuyaangalia matatizo na changamoto wanazopitia kama kikwazo kwao. Wanaona kwa yale wanayopitia, hakuna namna ambavyo wanaweza kutoka hapo na kufanya makubwa.
SOMA; Wajibika Ili Uachilie Breki Zinazokuzuia Kufanikiwa.
Kitu kibaya zaidi kwa wale wanaoshindwa ni kutafuta mchawi wa kushindwa kwao. Huwa wanatafuta mtu wa kumlaumu au kumlalamikia kwa yale mambo wanayokuwa wamepitia. Kwa kulaumu na kulalamika kwao wanakuwa wamejivua wajibu wa kujenga mafanikio makubwa.
Watu hawa wanaoshindwa huwa wanaona watu wengine ndiyo chanzo cha kushindwa kwao, kitu ambacho kimekuwa kinawafanya wabaki kwenye hali hiyo ya kushindwa kwa maisha yao yote. Kama watu hawa hawatapata bahati ya kufunguka ufahamu wao na kuyaangalia mambo kwa uhalisia wake, wanajikwamisha kabisa kufanikiwa.
Rafiki, sasa ni wakati wako wa kujua swali muhimu unalopaswa kujiuliza na kujijibu ili uweze kujenga mafanikio makubwa licha ya magumu ambayo unayapitia kwenye maisha yako kwa sasa. Fungua kipindi cha ONGEA NA KOCHA hapo chini na upate kujifunza, uchukue hatua na upate mafanikio makubwa.
Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani,
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi
0678 977 007 / amakirita@gmail.com
MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.