3379; Pakupeleka umakini wako.
Kutoka mezani kwa Kocha,
Rafiki yangu mpendwa,
Kwenye maisha yetu, kile tunachokipa umakini wetu ndiyo kinachokua zaidi.
Hiyo ina maana kwamba hakuna kitu chochote chenye nguvu kama hatujakipa sisi hiyo nguvu.
Umakini wetu, kwa maana ya kile tunachofikiri kwa muda mrefu ndiyo kunafanya vitu vipate nguvu.
Kukata tamaa kunapewa nguvu na sisi kuweka umakini wetu kwenye mambo yaliyopita, ambayo hatuna namna ya kuyabadili.
Sasa kwa sababu mambo yaliyopita hatuna njia ya kuyabadili, tunaona ndivyo maisha yote yalivyo, hakuna kinachobadilika.
Hofu inapewa nguvu na sisi kuweka umakini wetu kwenye mambo yajayo.
Kwa sababu bado hatujafikia mambo hayo, tunakuwa hatuna namna ya kuyaathiri na hivyo kujawa na hofu kubwa.
Hofu hizo zinakuwa hazina msaada kwa sababu hakuna unachoweza kwenye mambo hayo yajayo.
Matumaini yanapata nguvu kwa kuweka umakini kwenye wakati uliopo.
Kwa kufikiria kile kilocho mbele yako kwa wakati, unaona nini cha kufanya kwenye huo wakati ili matokeo yaweze kuwa mazuri.
Kwenye kila changamoto ambayo mtu unakuwa unapitia, huwa kuna tatizo na kunakuwa na fursa.
Kipi kinakuwa na nguvu zaidi inategemea fikra zako unapeleka wapi.
Ukipeleka umakini wako kwenye matatizo, hayo ndiyo yataonekana kuwa na nguvu zaidi.
Wakati ukipeleka umakini wako kwenye fursa zilizopo, utaweza kuona jinsi ya kunufaika na fursa hizo zaidi na zaidi.
Uzuri ni kwamba sisi wenyewe ndiyo wenye udhibiti wa fikra na umakini wetu.
Hivyo tunayo nguvu ya kuamua kipi kitawale fikra zetu mara zote na kukitumia kufanya makubwa.
Kwenye jamii ya KISIMA CHA MAARIFA, ambayo ni jamii ya tofauti tunayoijenga, tunakazana sana kulinda fikra zetu.
Haturuhusu chochote kisichokuwa sahihi kupata nafasi kwenye fikra zetu.
Tunahakikisha akili zetu zinakuwa safi muda wote ili kufikiri kwa usahihi yale yenye tija.
Ndani ya KISIMA CHA MAARIFA tunaweka umakini wetu kwenye wakati uliopo na fursa zilizo ndani ya kila kitu.
Tunaangalia nini tunaweza kufanya kwenye kila hali na hapo ndipo tunapoweka umakini wetu wote.
Uzuri ni unao udhibiti wa fikra zako na hivyo unaweza kuwa na udhibiti wa kila kitu kwenye maisha yako.
Tumia vizuri nguvu ulizonazo kufanya makubwa kwenye maisha yako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe