3388; Usiombe msamaha.
Kutoka mezani kwa Kocha,
Rafiki yangu mpendwa,
Hatua muhimu na ngumu kwenye safari yako ya kupata mafanikio makubwa ni kupambana kuwa huru.
Jamii uliyopo inakazana kuchukua uhuru wako, ili ikupelekeshe vile inavyotaka badala ya wewe kuyaishi maisha yako.
Jamii inajua ukiwa huru na kuyaishi maisha yako hutatawalika na hivyo haitaweza kujinufaisha kupitia wewe.
Katika kukamata uhuru wako, jamii inayokuzunguka hutumia kila njia.
Moja ya njia ambazo imekuwa inatumia sana ni ya kukufanya ujione ni mwenye hatia pale unapoyaishi maisha yako.
Jamii inakufanya ujione ni mkosaji sana kwa kuyaishi maisha yako hivyo unapaswa kuomba msamaha.
Jamii inajua ukishaomba msamaha, unakuwa umeingia kwenye mfumo wake wa kukutawala.
Hivyo hicho ni kitu ambacho unapaswa kukiepuka sana.
Ili kupata mafanikio makubwa, anza kwa kuwa huru kuyaishi maisha yako kwa namna ambayo ni sahihi kwako.
Kamwe usiombe msamaha kwenye mambo haya;
1. Kusema ukweli.
2. Kutenga muda kwa ajili yako.
3. Kuchukua hatua za hatari na kushindwa.
4. Kusema yale unayotaka kusema.
5. Kupumzika.
6. Kutenga muda na watu muhimu kwako.
7. Kutenga muda wa kujiandaa.
8. Kwenye yale unayoamini.
9. Kuepuka watu wasio sahihi kwako.
10. Kusema hapana.
Jamii itakufanya uone hayo mambo ni mabaya kwako kufanya hivyo unapaswa kuomba msamaha ili ikutawale.
Kamwe usiombe msamaha kuyaishi maisha yako.
Kama kuna makosa unakuwa umeyafanya kwenye kuishi mambo hayo, yamiliki makosa hayo na kuyarekebisha ili kupata matokeo bora.
Lakini kamwe usiombe msamaha kwa sababu watu wanakutaka ufanye hivyo.
Hayo ni matatizo yao na siyo yako.
Tingwa sana na kuyaishi maisha yako kiasi cha kukosa nafasi ya kuwaruhusu wengine wakutawale.
Kwenye jamii ya KISIMA CHA MAARIFA, ambayo ni jamii ya tofauti tunayoijenga, hatukubali kukubali hatia tunayotengenezewa kwa kuchagua kuyaishi maisha yetu.
Kipaumbele chetu ni kuyaishi maisha yetu kwa namna sahihi kwetu.
Na kama kuna ambao wanakwazika na sisi kuishi maisha yetu, hizo ni shida zao.
Hatuwapangii wengine jinsi ya kuishi maisha yao na hivyo pia hatuwapi nafasi ya kutupangia maisha yetu.
Tunajua tunachotaka, tunao mchakato wa kukipata, wajibu wetu ni kukaa kwenye mchakato huo kwa msimamo na kupuuza mengine yote.
Hivyo ndivyo tunavyojihakikishia mafanikio makubwa kwenye maisha yetu.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe