Rafiki yangu mpendwa,

Maisha yana mtego mkali sana.

Unapokuwa unaanzia chini kabisa, unakuwa tayari kufanya shughuli yoyote halali ili kuyajenga maisha yako.

Hilo linakusukuma wewe kujituma sana, kitu kinachopelekea uweze kutoka chini na kuanza kupanda juu.

Unapopanda juu, unakuja kugundua kwamba shughuli ambazo uliingia awali hazikuwa sahihi kwako.

Mwanzo hukuwa na namna nyingine, ilikubidi ufanye ili uweze kutoka chini. Lakini baada ya kutoka chini, unakuwa unatamani maisha yako yawe na uhuru, kitu ambacho kinakuwa kigumu.

Hivyo ndivyo watu wengi wanajikuta wakiwa kwenye kazi au biashara ambazo zinawanyima kabisa uhuru. Kazi au biashara hizo zinakuwa zinawalipa vizuri, lakini zinawanyima uhuru wa kuyaishi maisha yao kwa namna wanavyotaka wao.

Lakini pia kunakuwa na kitendawili kingine, watu hao wanakuwa hawawezi kuacha kazi au biashara hizo kwa sababu ndiyo wanazitegemea kuyaendesha maisha yao. Hivyo wanakuwa ni kama wamenasa kwenye mtego mkali, wanataka kuwa huru, lakini pia wana utegemezi kwenye kile wanachotaka kuachana nacho.

Ipo njia ya kuweza kuondoka kwenye kazi au biashara ambayo inakunyima uhuru. Njia hiyo inakutaka wewe kuyapitia upya maisha yako na kuondoa baadhi ya vitu ambavyo ndiyo vinakukwamisha kuwa huru.

Sehemu kubwa ya mizigo ambayo umejibebesha kwenye maisha yako, unaweza kuitua na ukaweza kupata uhuru mkubwa wa maisha yako. Umekuwa unaendelea kung’ang’ana na mizigo hiyo kwa sababu hujawahi kuona jinsi maisha yako yanavyoweza kuwa bora kwa kuitua hiyo mizigo.

Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA nimekupa mpango mzima wa jinsi unavyoweza kuondoka kwenye kazi au biashara ambayo inakunyima uhuru. Karibu ujifunze kwa kuangalia kipindi hicho hapo chini.

Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani,

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi

0678 977 007 / amakirita@gmail.com

www.amkamtanzania.com

MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.