
Katika mji mmoja alikuwepo mfanyabiashara mgeni, aliyehamia na kufanya biashara. Mfanyabiashara huyo alikuwa mtu wa watu, hakuwa na pesa nyingi sana, lakini wanakijiji walimpenda.
Katika mji ule kulikuwa na kituo cha watoto wenye uhitaji. Hivyo, mara moja moja alikuwa anatoa msaada wa bidhaa kidogo kutoka dukani kwale. Hali hiyo ilifanya wakazi wazidi kumpenda sana. Alikuwa mstari wa mbele kusaidia wenye majanga, watu wenye huitaji kulingana na uwezo wake. Alifanya hivyo kwa muda wa miaka mitatu.
Baada ya miaka mitatu biashara yake ikaanza kukua kwa kasi, wateja wakaongezeka siku hadi siku. Wafanya biashara wa pembeni wakaanza kunongonezana namna gani mfanyabiashara mwenzao mchawi na mengine mengi.
Kwakuwa hakuwa mkazi wa pale, muda wa kuondoka ulifika. Akatafuta mteja na kumuuzia bidhaa zote. Kabla ya kuondoka baadhi ya watu, akiwemo mnunuzi wa bidhaa zake walitaka kujua siri ya mafanikio ya biashara yake. Mfanyabiashara huyo, alisema, ni kulipa fadhila. Hiyo ndiyo siri. Akaongezea, sina pesa nyingi, lakini niliwapenda wanakijiji na sikuwahi kuwa na majigambo. Niliishi maisha waliyoishi, nilitoa zawadi na mengine mengi. Zawadi waliyonipa wao ni kuja kununua kwangu. Àsante sana.
Kitu tunachojifinza katika hadithi hii ukiachana na mengine mengi ni fadhila. Kwanini fadhila, na ilimsaidiaje kuongeza ushawishi?
Ipo hivi, sisi binadamu ni viumbe wa hisia tunashawishika haraka na mtu anayejali anatujali. Sio tu eneo la fedha tu, lakini akifanya tujisikie vizuri, ni rahisi kuwa karibu naye.
Kama muuzaji bora kuwahi kutokea, ipo namna nzuri ya kutumia nyenzo ya fadhila kuongeza ushawishi kwa wateja unao wahudumia. Hapa chini nimeainisha mambo ya kuzingatia;
Moja; Wasaidie wengine, kupata wanachotaka.
Hata kama mtu hakupendi, lakini akikumbuka ulimsaidia, atakuwa tayari kukusaidia. Maana tayari ameishapata kile unachotaka.
Mbili; Wape zawadi.
Saikolojia nyuma ya zawadi ni kwamba, mtu akipokea zawadi anajiingiza deni. Hivyo, unapotaka akusaidie inakuwa rahisi kushawishika. “Zawadi ikiendana na mtu unayempa inakuwa na ushawishi sana”. Rejea mfano wa muuza karanga. Hii pia wafanyabiashara wanaifanya sana.
Tatu; Omba, Omba tena.
Hapa unaweza kuanza na ombi kubwa kulingana na uhitaji wako, akikataa ombi kubwa, omba ombi dogo. Sio rahisi mtu akatae ombi kubwa na dogo kwa pamoja.
Tahadhali, usitoe fadhila kubwa kwa hisia kisa ulisaidiwa, tafakari vizuri kisha ufanye maamuzi sahihi.
Wakati ndio huu kutumia nyenzo hii ya fadhila kuongeza ushawishi katika biashara yako. Kumbuka maisha ya sasa ni ya “nipe nikupe“, kile unachofanya Kwa mteja ndicho anakufanyia. Je, unamfanyia nini? Ni swali la kufanyia kazi.
Imeandaliwa na Lackius Robert Mkufunzi Msaidizi Chuo Cha Mauzo na Mwandishi. Tuwasiliane 0767702659 au mkufunzi@mauzo.tz.
Muhimu; Kama bado biashara yako ina changamoto ya mauzo kuwa madogo, wateja wachache tunalo suluhisho lako. Karibu CHUO CHA MAUZO TANZANIA.