Rafiki yangu mpendwa,

Hebu pata picha kama ungekuwa huna hofu kabisa,

Ni mambo gani makubwa ambayo ungeweza kuyakamilisha kwenye maisha yako?

Si ungekuwa umepata kazi ya ndoto yako na kupatana mshahara mkubwa kama ambavyo umekuwa unataka?

Si ungekuwa umeanzisha biashara ya ndoto yako na kuikuza sana?

Si ungekuwa umeoa au kuolewa na mtu wa ndoto yako na unayafurahia maisha?

Rafiki, hofu imekuwa inatukwamisha sana kwenye maisha.

Tunajua kabisa nini tunachotaka na tunajua kabisa nini tunapaswa kufanya ili kupata tunachotaka.

Lakini unapofika wakati wa kufanya, hofu inatuzuia.

Tunapata picha ya mambo kwenda vibaya na kuona bora tuache kwanza, maana bado hatujawa tayari.

Na hivyo ndivyo tunavyokuwa tunayakosa maisha ya ndoto yetu.

Maana maisha huwa hayasimami kukusubiri, yanaendelea kwenda mbele na kukuacha wewe nyuma.

Rafiki, vipi kama nikikuambua ipo dawa ya wewe kuondokana na hofu kabisa.

Vipi kama nikikuhakikishia kwamba unaweza kuitokomeza kabisa hofu kwenye maisha yako.

Je utakuwa tayari kulipa gharama kiasi gani kuipata dawa hiyo?

Utakuwa haraka kiasi gani kuchukua hatua ili uweze kuondokana na hofu na kujizuia kuishi maisha ya ndoto yako?

Najua utakuwa tayari kuchukua hatua, maana umechoshwa na maisha unayoishi sasa, ambayo ni tofauti kabisa na ndoto ulizokuwa nazo.

Rafiki, habari njema sana nilizonazo kwako ni kwamba hiyo njia ipo na haihitaji wewe ulipe gharama yoyote ile.

Kinachohitajika ni wewe tu uijue njia, kisha kuifanyia kazi.

Na hapo matokeo unaanza kuyaona mara moja.

Huhitaji hata kusubiri muda mrefu ndiyo njia ianze kufanya kazi.

Ni unaifanyia kazi na mara moja matokeo unaanza kuyaona.

Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA hapo chini nimekuelezea dawa hiyo kwa kina, kwa namna ambayo kazi yako ni kuchukua hatua tu.

Acha kila unachofanya sasa na angalia kipindi hicho na ondoka ukaanze kufanyia kazi hiyo dawa unayokwenda kujifunza hivi punde. Karibu ujifunze na uchukue hatua ili kutokomeza kabisa hofu kwenye maisha yako na kuishi maisha ya ndoto yako.

Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani,

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi

+255 678 977 007 / amakirita@gmail.com

www.amkamtanzania.com

MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.