3424; Chora Mstari.
Kutoka mezani kwa Kocha,
Rafiki yangu mpendwa,
Matatizo yote tunayokutana nayo kwenye maisha yetu huwa yanatokana na watu.
Ni wale watu wanaotuzunguka ndiyo wenye nguvu ya kuyaathiri sana maisha yetu.
Sehemu kubwa ya athari ambazo tunakuwa nazo kwenye maisha yetu ni kuruhusu watu wengine kufanya maamuzi kwa niaba yetu.
Hapa watu wanaotuzunguka wanakuwa ni wengi na tunawaamini na kuwapa mamlaka ya kufanya maamuzi.
Kwa sehemu kubwa maamuzi ambayo yamekuwa yanafanyika kwenye hizo hali yanakuwa ni maamuzi ya mazoea.
Maamuzi hayo ya mazoea yanafanyika kwa sababu watu wanakuwa tayari kupokea chochote.
Kunakuwa hakuna viwango vilivyowekwa ambavyo kila aliyepo anapaswa kuvifikia.
Matokeo yale ni kila mtu anajikuta akiweza kupata nafasi ya kushauri au kuamua mambo mbalimbali.
Ili kuboresha matokeo unayoyapata, unapaswa kuanza kwa kuweka viwango ambavyo vitaamua nani anapata nafasi na nani hapati nafasi.
Kuweka viwango sahihi, anza kwa kuchora mstari wa nani anapata nafasi na nani hapati nafasi kwenye maisha yako.
Mstari unaochora unatenganisha wale wanaoyafanya maisha yako kuwa bora na wasiokuwa na mchango.
Wanaochangia kuyaboresha maisha yako wanapata nafasi, wakati ambao hawana mchango wanakosa nafasi.
Ukishachora mstari, unasimamia huo na hakuna upendeleo wowote unaoruhusu wasiokuwa sahihi.
Ni mtu anakuwa na mchango wa kuyafanya maisha yako kuwa bora au kutokuwa na mchango.
Hivyo mtu anapata nafasi kulingana na mchango wake.
Watu ni wengi kwenye maisha, huwezi kuwapa wote nafasi sawa wakati kuna ambao wana mchango mkubwa kuliko wengine.
Kwa wale ambao hawana mchango kwenye kuyafanya maisha yako kuwa bora, wanatakiwa kuonyeshwa mlango wa kutokea haraka sana.
Muda wako ni mchache, utumie na wale wanaokubali na kuwa na mchango mkubwa kuliko wengine.
Wewe ndiye wa kuamua nani wa kumruhusu na nani wa kumnyima.
Ukishaweka vigezo ambavyo unawachuja navyo watu, hivyo ndiyo unapaswa kuvizingatia wakati wote na watu wote.
Ondoa kila aina ya upendeleo ili kufanya maamuzi sahihi na kupata matokeo bora.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe