Rafiki yangu mpendwa,
Siri kuu ya kujenga utajiri ni ubahili.
Lakini ubahili ni neno ambalo watu wengi huwa hawapendi kulisikia.
Hiyo ni kwa sababu neno hilo limepewa kasumba mbaya.
Ubahili huwa unaonekana ni mtu kujitesa licha ya kuwa na fedha.
Yaani uwe na fedha lakini ushinde njaa, au uvae nguo za hadhi ya chini.
Na mengine kama hayo.

Lakini huo siyo ukweli, maana halisi ya ubahili siyo kujitesa.
Maana halisi ya ubahili ni matumizi kuwa chini ya kipato.
Kama kipato ni milioni moja, matumizi yawe chini ya hapo.
Mengine ya unafanyaje sasa ndiyo inakuwa juu yako. Lakini unachotakiwa ni kuhakikisha matumizi unayofanya hayazidi kipato unachoingiza.
Hivyo basi, kama unataka kufanya matumizi zaidi, hakuna anayekuzuia, kwani unaweza kuongeza kipato chako kadiri ya unavyotaka.
Unachotakiwa ni kuhakikisha tu kwamba matumizi yako hayazidi kipato.
Hivyo kama unaona ubahili unakubana usitumie vile unavyotaka, unaruhusiwa kuongeza kipato chako kadiri unavyotaka ili kikidhi mahitaji yako.
SOMA; Kujenga Utajiri Kupitia ARDHI Na AKIBA.
Kitu ambacho watu wamekuwa wanashangaza na kinawaweka kwenye umasikini ni kuwa na matumizi makubwa kuliko vipato vyao. Hivi unadhani kama kipato chako ni milioni moja, lakini matumizi yako ni zaidi ya milioni moja, hiyo ziada uliyotumia umeitoa wapi?
Hapo unakuwa umetumia fedha ambayo huna na dunia huwa inakuadhibu kwenye hilo. Kwani unapokopa fedha, huwa unailipa kwa riba ambayo inazidi kuongeza matumizi yako.
Swali ambalo unaweza kuwa unajiuliza ni unawezaje kukidhi matumizi yako chini ya kipato chako ambacho pia hakitoshelezi?
Nimejibu swali hilo kwa kina kabisa kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA hapo chini. Karibu ujifunze kwa kina kwenye kipindi hicho ili uweze kuelewa na kutumia vizuri ubahili kujenga utajiri mkubwa kwenye maisha yako.
Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani,
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi
+255 678 977 007 / amakirita@gmail.com
MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.