Anaitwa Jeb Blount ni mwandishi na muuzaji bora wa kipindi kirefu, moja ya andiko lake katika kitabu cha “Fanatical Prospecting” anasema, “yalikuwa maneno kumi na moja, sikumbuki vema niliyasikia wapi ila kati ya hayo, ni moja tu ninalokumbuka. Neno hilo linasema, “make one more call” likiwa na maana, piga simu moja zaidi. Neno hili limebadili maisha yangu”.


Jeb anasema, neno hili nililiandika katika meza yangu kama falsafa ya kutumia. Lilikuwa neno la mwisho kutazama kabla sijaenda mahali popote au kupiga simu.

Nilipokuwa nahisi uchovu nilikuwa ninapiga simu moja zaidi, ninafanya kazi mara moja au kumtembelea mteja mmoja zaidi.

Wakati mwingine nimejikuta ninapofanya mara moja zaidi ninanogewa. Kama ni simu zinakuwa tatu au nne.

Hali iliyonisaidia kukuza mauzo na kuweka ukaribu na  wateja wangu.  Nakushauri na wewe uzingatie falsafa hii, ili ukuze mauzo yako.

Je, falsafa ya moja zaidi inamaanisha nini kwetu wauzaji bora kuwahi kutokea?

Inamaanisha tuongeze hatua moja zaidi katika utendaji na ufuatiliaji wetu.

Ni kweli tunakutana na hali tofauti zinazofanya tuchoke, tunapoanza kuchoka huwa tunatamani  kufanya vitu vyetu siku inayofuata.

Na hapo ndipo tunasema, nitafanya kesho, nitaongea naye kesho, nitamtembelea kesho.

Tunasahau, kesho pia huwa na matokeo yake. Lakini kutumia falsafa ya moja zaidi itakusaidia sana.

Wakati mwingine tunaweza kuona vitu tunavyofanya havileti manufaa au kutufikisha mahali fulani.

Lakini ukiwa na falsafa hii itakusaidia kuongeza chachu kwenye kazi zako.

Kabla hujaacha unachofanya ongeza moja zaidi. Uza kwa mteja mmoja zaidi.

Hata kama unahisi kuchoka. Uambie moyo wako ngoja nitafute mteja, niwasiliane mara moja zaidi.

Utapata matokeo makubwa maana ni falsafa iliyowasaidia wengi.

Faida za kutumia falsafa hii;

Moja; Inakusaidia kukupa hamasa katika utendaji wako

Mbili; Inakusaidia kujiondoa kwenye sababu

Tatu; Inakusogeza karibu na wateja wengi.

Ni wewe kuitumia falsafa hii kwa msimamo bila kuacha. Iwe wakati wa mvua au jua. Fanya mara moja zaidi.

Hatua za kuchukua leo; Kwa kila jukumu unalofanya, kabla hujaacha fanya mara moja zaidi.

Mfano, kama ni utembeleaji, tembelea mteja mmoja zaidi. Kama ni simu, piga simu moja zaidi. Baada ya siku 90 utapata matokeo makubwa.

SOMA: Tumia Mapungufu Ya Mteja Kukamilisha Mauzo

Je, ni falsafa ipi inakuongoza katika utendaji wako?

Shirikisha hapa tujifunze kitu kutoka kwako.

Asante sana karibu ufanyie kazi katika yale uliyoweza kujifunza kwenye somo hili.

Wako Wa Daima

Lackius Robert

Mkufunzi Wa Mauzo na Mwandishi

0767702659 /mkufunzi@mauzo.tz

Karibu tujifunze zaidi.