Kwenye maisha na utendaji wetu, kuna namna tumekuwa tunashindwa kukamilisha vitu, tukiamini tutavikamilisha baadaye.

Baadaye hiyo inapofika, tunajikuta tuna mrundikano wa vitu ambavyo kuvimaliza kwa wakati huo, inakuwa ngumu.


Hapo ndipo wengi wetu tunaanza kuchagua vitu vichache vya kufanya kuisogeza siku yetu. Licha ya kuvichagua vitu hivyo, lakini bado hatuvikamilishi.

Chanzo kikubwa cha uwepo wa vitu hivyo ni ughairishaji, ambao umetokana na kuacha hewani baadhi ya majukumu au kazi tulizokuwa tunafanya.

Hali inayopelekea kukosa utulivu na kufanya makosa mengi kwa sababu ya kutaka kukamilisha majukumu kwa uwepesi. 

Unachopaswa kujua ni kwamba, ughairishaji ni adui mkubwa wa uzalishaji na mafanikio.

Hii ni kwa sababu mghairishaji anaacha mambo ya msingi, anakaribisha sababu, anafanya vitu kwa kuangalia matokeo ya muda mfupi.

Hali inayopelekea huduma na mauzo kuwa duni.

Ili ufanikiwe kuwa muuzaji bora kuwahi kutokea na kutoa huduma bora kwa wateja wako fuata njia hizi kuushinda ughairishaji;

Moja; Weka malengo yanayopimika.
Kutumia kanuni ya SMART( Specific, measurable, achievable, relevant, and time bound).
Hii itakuwa kama dira yako kwenye kila jambo unalofanya, ili iwe rahisi kulikamilisha.

Mbili; Gawa majukumu katika makundi au hatua  ndogo ndogo.
Mfano, kama ni simu 100 zigawe 20 kila saa moja. Lengo ni kutoona na nyingi na kushindwa kuzikamilisha.

Tatu; Kuwa na ratiba inayokuongoza.
Unaweza kuweka malengo ndiyo, lakini kama hamna ratiba nzuri kufanya vitu kwa mpangilio utajikuta unafanya vitu vingi vyenye matokeo kidogo.

Nne; Jitoe katika mazingira yanayopelekea kughairisha mambo. Inaweza kuwa ni upande matumizi makubwa ya mitandao ya kijamii, mpira au vitu vingine.

Tano; Fanya kwanza kabla ya kulalamika
Kiasili binadamu tu wavivu. Kazi yoyote mbele yetu, lazima tulalamile kwanza kabla ya kuifanya.

Ukiweka utaratibu wa kuwa mtu wa kufanya utajikuta unapunguza majukumu na inakupa urahisi wa kujifunza sehemu unazokwama.

Hatua za kuchukua leo; Jipe changamoto ya kukamilisha jukumu lisilozidi dakika ya mbili kulikamilisha.

Ikiwa na maana kama jambo linaweza kufanyika ndani ya dakika mbili usiliache hewani. Hi ni kanuni iliyotolewa na Mwandishi David Allen katika kitabu cha Getting the things done. Inaitwa kanuni ya dakika mbili.

Ifanye kwa siku 90 hadi miezi sita, utaona matokeo makubwa.

SOMA; Tumia Kanuni Ya A, B, C, D na E Kufanikisha Vipaumbele Vyako Na Kuwauzia Wateja


Je, ni wateja au oda ngapi umezikosa kisa ughairishaji?

Wako Wa Daima

Lackius Robert

Mkufunzi Wa Mauzo na Mwandishi

0767702659 / mkufunzi @mauzo.tz

Karibu tujifunze zaidi.