Rafiki yangu mpendwa,
Kila mtu anapenda utajiri kwenye maisha yake.
Japo kuna wanafiki ambao huwa wanasema hawataki utajiri, kinachowakosesha usingizi na hata amani kwenye maisha yao ni fedha.
Hivyo watu hao wangeweza kuwa na utulivu zaidi kama wangekuwa na fedha zaidi. Ndani yao wanataka utajiri, hata kama nje wanasema tofauti.
Watu pia wanaweka juhudi mbalimbali ili kupata utajiri. Kwa mfano watu wanafanya kazi au biashara zao kwa muda mrefu, wanaweka juhudi sana ili kuongeza kipato chao.
Wengi pia juhudi wanazoweka zinawaongezea kipato, na huenda kipato hicho kikafanya maisha yao kuwa mazuri, lakini bado wanashindwa kujenga utajiri.
Licha ya kuwa na kipato kikubwa, bado wengi wanashindwa kujenga utajiri kwa sababu kipato siyo utajiri. Yaani kuweka juhudi kubwa na ukaongeza kipato, haimaanishi kwamba utakuwa tajiri.

Kujenga utajiri ni kazi ya tofauti kabisa, kazi ambayo inajitegemea yenyewe na inapaswa kuwekewa juhudi za tofauti.
Wengi wanaoingiza kipato kikubwa wamekuwa hawajengi utajiri kwa sababu hawajui ni kazi iliyokamilika na inayopaswa kuwekewa juhudi zake. Wengi wanadhani kipato kikubwa pekee kinatosha, lakini hilo linawakwamisha sana.
Kwa sababu wajibu wangu ni kuhakikisha wewe rafiki yangu unapata maarifa sahihi kabisa na kuyafanyia kazi ili kufanikiwa, nimekueleza kazi kubwa ya kujenga utajiri iko wapi na nini unachopaswa kufanya ili kupata utajiri huo.
Yote hayo nimekueleza kwa lugha rahisi kabisa kwako kueleweka kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA hapo chini. Tafadhali fungua kipindi hicho, jifunze na chukua hatua ili uweke juhudi sahihi na ujenge utajiri.
Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani,
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi
+255 678 977 007 / amakirita@gmail.com
MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.