3440; Kufanya hata kama hujisikii kufanya.

Kutoka mezani kwa Kocha,

Rafiki yangu mpendwa,
Kitu kimoja kitakachokuhakikishia matokeo bora ni kuweza kufanya yale uliyopanga, hata kama hijisikii kufanya.

Kila mtu huwa ni mzuri sana kwenye kuweka mipango ya kufikia malengo ambayo yapo.
Lakini unapifika wakati wa kutekeleza yale yaliyopanga, ndiyo shida huanza.

Kuanza kufanya jambo lolote, hasa linapokuwa jipya na lenye manufaa, huwa kunavutia mwanzoni.
Lakini kwenye ufanyaji, mtu huwa anakutana na changamoto na vikwazo mbalimbali.

Hapo kwenye changamoto na vikwazo ndipo panapowatofautisha wanaofanikiwa na wanaoshindwa.
Wanaofanikiwa huwa wanaendelea kufanya bila ya kujali wanajisikia kufanya au la.
Wanaoshindwa huwa wanaendeshwa na mihemko, wakijisikia kufanya wanafanya, wasipojisikia kufanya hawafanyi.

Kwa sababu ni mara chache sana mtu kuweza kujisikia vizuri kwenye kile anachofanya, inakuwa vigumu pia kwa mtu kufanya makubwa kadiri ya anavyokuwa anataka.

Ukiruhusu hisia au vikwazo kuwa ndiyo vinaendesha maanuzi na tabia zako, unakuwa unajizuia mwenyewe kufanikiwa.

Kuwa mtu wa kupanga na kufanya bila ya kuruhusu hisia zozote kukuingilia na kukukwamisha.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe