Habari njema muuzaji bora kabisa kuwahi kutokea,

Karibu sana kwenye mwendelezo wa makala zetu za ukamilishaji ambazo ni mwendelezo wa makala kutoka kwenye programu yetu ya  CHUO CHA MAUZO.

Hongera sana kwa kuendelea kujifunza na kuchukua hatua kwa haya unayoendelea kujifunza hapa.

Leo ni jumatano ya ukamilishaji tukiongozwa na kauli mbiu yetu inayosema ABC ALWAYS BE CLOSING-MARA ZOTE KUWA UNAKAMILISHA WATEJA.

Kama kauli mbiu inavyosema, mara zote unapaswa kukamilisha wateja na wewe pia unapaswa kukamilisha wateja. Na kukamilisha ndiyo wajibu wako namba moja kwenye biashara yako.
Wajibu wako namba moja ni kuuza na unapokuwa umemuuzia mteja maana yake umemkamilisha.
Hivyo basi, kila wakati wageuze wateja tarajiwa uliokuwa nao na waweze kununua na kuwa wateja kamili.

Ukamilishaji ndiyo kitu muhimu sana kwenye mauzo kwa sababu ndiyo kitu pekee kinacholeta fedha kwenye biashara kupitia kile unachouza iwe ni bidhaa au huduma.

Kwenye somo letu lililopita tulijifunza mbinu mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo nayo ni mbinu namba 43 na 44

Kwenye mbinu namba 43 tulijifunza ukamilishaji wa ndiyo tatu na basi.
Na kwenye ukamilishaji wa namba 44 tulijifunza ukamilishaji wa rufaa.

Na kwenye ukamilishaji wa ndiyo tatu basi, mbinu namba 43 tulijifunza kwamba ndiyo ni neno lenye nguvu kubwa, muulize mteja maswali atakayojibu ndiyo kisha kamilisha mauzo.

Na kwenye ukamilishaji wa rufaa, tulijifunza kwamba ukamilishaji wa rufaa unamfanya mteja aonene ana nguvu ya majadiliano, kwa kukupa watu zaidi anaona atapata punguzo. Pia, watu wanapenda kuwasalimu wengi, wakiamini kwa kufanya hivyo na wao watasaidiwa.

SOMA; Mbinu Mbili Za Uhakika Za Ukamilishaji Wa Mauzo 43-44

Leo kwenye jumatano ya ukamilishaji tukiongozwa na kauli mbiu yetu inayosema ABC ALWAYS BE CLOSING-MARA ZOTE KUWA UNAKAMILISHA WATEJA, tunakwenda kujifunza mbinu nyingine mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo nazo ni mbinu namba 45 na 46.

Zifuatazo ni mbinu mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo ambazo tunakwenda kujifunza hapa;

45. Ukamilishaji wa malipo kidogo.

Kwa ukamilishaji huu unagawa bei ya kitu kwa muda ambao atakitumia na kumwonyesha mteja ni malipo kidogo anafanya.

Kwa mfano kama ni kitu cha milioni 3, ambacho atatumia kwa miaka kumi, kwa mwaka ni kama laki tatu na kwa mwezi ni kama elfu 25.
Kwa kugawa hivyo mteja anaona analipia kidogo.

Mteja anakuambia malipo ni makubwa sana kama pingamizi na wewe unamwambia mteja hivi;
“Kwa malipo kidogo ya … kila mwezi, unakwenda kupata bidhaa/huduma hii bora na yenye manufaa makubwa kwako.”
Kinachofuata baada ya hapa ni wewe kukamilisha malipo ili uende kufurahia uwekezaji wako.

46. Ukamilishaji wa kuigeuza namba kuwa ndogo sana.

Huu ni ukamilishaji wa kutumia kwenye pingamizi la bei, mara zote gawa bei kwa kiwango ambacho ni kidogo na mteja kuona anaweza kukimudu.

Mara nyingi kinachowakwamisha wateja siyo kutokumudu, bali namba kubwa wanayoiona. Igawe ionekane ndogo kwao na kamilisha mauzo.

Kwa mfano, mteja baada ya kukupa pingamizi la bei, unamjibu hivi kwa ukamilishaji huu;
“Milioni moja kwa mwezi ni elfu 30 tu kwa siku. Kwa kiasi hicho unakwenda kupata bidhaa/huduma hii bora kabisa kwako.”

Kinachofuata baada ya hapa ni wewe kukamilisha malipo, kamilisha malipo, weka sahihi yako hapa, Rafa lipia.

Ukamilishaji wa mauzo ni pale mteja anapokubali kutoa fedha na kupata bidhaa au huduma unayouza. Kama mteja hajafanya maamuzi hayo, mauzo hayajakamilika, hata kama ameahidi kwa msisitizo kiasi gani.

Ni mpaka mteja aseme nimekubali kununua na kutoa fedha au mpango wa malipo ndiyo mauzo yamekamilika. Hivyo hatua ya ukamilishaji ni muhimu sana kwenye mchakato wa mauzo, kwani ndiyo inayoleta mafanikio au kushindwa kwenye mauzo. Kwa sababu ushindi kwenye mauzo unapimwa kwa wale waliokubali pekee na siyo kwa ahadi.

Nenda leo ukawe mkamilishaji bora kabisa kuwahi kutokea na ukauze zaidi.
Shika kichwa chako na jiambie kauli hii;  Mimi … (Taja jina lako)
Ni muuzaji bora kuwahi kutokea.
Mimi ni mkamilishaji bora wa mauzo na leo ninakamilisha mauzo ya Tsh….Taja kiasi kwa kila mteja niliyemweka kwenye mchakato wa mauzo

Kutoka kwa muuzaji mwenzako, rafiki anayekupenda na kukujali,

Mwl.Deogratius Kessy

Mwalimu/Mwandishi/Mjasiriamali
Makamu Mkuu wa CHUO CHA MAUZO.
makamu@mauzo.tz, 📞0717101505//0767101504