Rafiki,
Umewahi kuona mtu anayeumwa, lakini kila mkimwambia aende hospitali kupata matibabu anakataa.
Anaanza kusema; Oh! nitakuwa sawa ngoja nisikilizie kesho nitakavyoamka. Lakini majira ya saa nane usiku hali inavyozidi kwa maana ya kukohoa au kuharisha damu anavyokuwa mpole na kuomba awahishwe hospitalini kupata matibabu!
Au mtu mwingine anayo njaa kweli kweli na pesa anayo lakini akakaa na njaa yake hadi jioni. Njaa inapozidi kunakuwa hakuna jinsi anaitumia haraka na kupata chakula.

Hali hiyo ipo pia, kwenye mauzo.
Mteja anaweza kuwa na uhitaji wa kitu kabisa lakini asifanye maamuzi ya kukichukua. Ni mgonjwa anaumwa lakini hataki kununua dawa.
Hili ni suala unalopaswa kulijua ili unapokutana na mteja uongeze nguvu ya kumshawishi ili afanye maamuzi ya kuchukua hitaji hilo.
Wauzaji wengi wamekuwa wanatumia muda mrefu kufanya mazungumzo na wateja bila kujua mahitaji yao, hali inayowafanya kuchelewa kuwauzia.
Kama muuzaji bora kuwahi kutokea ni vema jitahidi kujua mahitaji ya mteja kwa kuzingatia yafuatayo;
Moja; Msikilize mteja
Wauzaji tunasifika kwa kuwa waongeaji sana kuliko kusikiliza. Hali inayopelekea kutojua hitaji la mteja.
Unaposikiliza unaelewa haraka na kujua hitaji la mteja wako. Maana, anakuwa anazungumzia kitu kinachomsumbua.
Mbili; Muulize maswali
Huwezi kuuliza maswali sahihi kama hujasikiliza kwa umakini. Hivyo, mbele ya mteja sikiliza na uliza maswali mkakati.
Wakati wa kuandaa maswali hakikisha unauliza maswali yanayokusogeza au kukupeleka kwenye mauzo.
Tatu; Mpe ushuhuda
Moja ya faida ya ushuhuda ni kumfanya mteja aone kuna wateja waliofanya maamuzi au manunuzi kabla yake.
Hii inamjengea imani mteja na kushawishika haraka kukamilisha mauzo.
Nne; Mpe “Summary” ya mazungumzo mliyofanya. Hapa chagua maeneo machache yenye uzito kulingana na mazungumzo yenu au maumivu ya mteja.
Summary kinakusaidia kumpatia suluhisho au maslahi atakayopata baada ya kutumia bidhaa au kujiunga na huduma yako.
Tano; Mpe hatua za kuchukua.
Hatua zinaweza kujaza fomu, kulipia bidhaa au huduma, kupanga mkutano mwingine.
Habari njema kuhusu kumpatia hatua za kuchukua ni kukusaidia kutoanza upya kila wakati.
Kitu muhimu ni kuepuka ni uvivu wa kutoa maelezo ya muhimu. Wewe ndiye unayejua bidhaa au biashara kwa kina.
Kama kuna maelezo ya msingi mpatie mteja, usiyabanie. Yanaweza kukusaidia kumuuzia.
SOMA; Tumia Nyenzo Za Uhaba Na Msimamo Ili Kuwa Na Ushawishi Mkubwa Kwa Wengine.
Hatua za kuchukua leo; Ainisha mahitaji yote muhimu kwa mteja unayemfuatilia, ili iwe rahisi kumsaidia kufanya maamuzi.
Wako Wa Daima
Lackius Robert
Mkufunzi Wa Mauzo na Mwandishi
0767702659 /mkufunzi@mauzo.tz
Karibu tujifunze zaidi.