Rafiki yangu mpendwa,

Watu wamekuwa wanaonyesha kwamba wana kiu kubwa ya mafanikio, lakini hawayapati mafanikio wanayokuwa wanayataka.

Na moja ya sababu wanazokuwa wanatoa kama kikwazo kwao kufanikiwa ni ule ushindani mkali unaokuwepo kwenye safari ya mafanikio.

Kila eneo linaonekana kuwa na ushindani mkali.

Kwenye kazi kuna ushindani mkali, kwa sababu nafasi za kazi ni chache lakini wanaotaka kazi ni wengi. Hilo limepelekea hata malipo yasiwe makubwa kama kipindi cha nyuma.

Kwenye biashara pia ushindani ni mkali, msukumo wa wengi kuingia kwenye biashara huwa ni kuona biashara nyingine zinazolipa na hivyo kujipeleka kwenye ushindani.

Na hata kama utakuja na wazo jipya na la kibunifu, kama litafanya vizuri wengine wataiga na hivyo kuwa umekaribisha ushindani.

Japo kuna huo ushahidi wa wazi kwamba ushindani ni mkali, lakini huo siyo unaowakwamisha watu kufanikiwa. Ushindani unaoonekana kwa nje, ambapo unatokana na wengine siyo unaopelekea watu kushindwa.

Bali ushindani wa ndani ambao watu wameubeba ndiyo umekuwa kikwazo kwao kufikia mafanikio makubwa kwenye lolote wanalofanya.

Rafiki yangu mpendwa, kuna kitu kimoja ambacho kipo ndani yako na unakipenda sana ambacho ndiyo ushindani namba moja kwako. Kitu hicho ndiyo kimekuwa kinakuzuia kabla hata ushindani wa nje haujawa na madhara yoyote kwako.

Ukiweza kuona jinsi kitu hicho ulichozoea kinavyokuzuia, utaweza kukivuna na kufanya makubwa sana kwenye maisha yako.

Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA hapo chini nimeweza kukufafanulia kwa kina kuhusu kitu hicho cha ndani yako kinachokukwaza usifanikiwe.

Karibu ujifunze kuhusu kitu hicho na uchukue hatua za makusudi kuweza kufanya makubwa kwa kuvuka kila aina ya ushindani wa nje. Fungua hapo chini kujifunza.

Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani,

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi

+255 678 977 007 / amakirita@gmail.com

www.amkamtanzania.com

MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.