3447; Usiwape nguvu ya kukukwamisha.
Kutoka mezani kwa Kocha,
Rafiki yangu mpendwa,
Hakuna mtu yeyote anayeweza kukukwamisha kwenye maisha yako, kama wewe mwenyewe hujampa nafasi ya kufanya hivyo.
Unatoa nafasi ya vitu au watu kukusumbua pale unapovipa umuhimu mkubwa kuliko ambavyo vinastahili kupata.
Unapoona mambo hayawezi kwenda bila ya kuwepo kwa mtu au vifu fulani, unakuwa umeruhusu kukwamishwa.
Kuwa na mbadala wa kila kitu na kila mtu ili usikwamishwe kwa namna yoyote ile.
Kupuuza vitu au watu kwa kutokuwapa umuhimu usiostahili ni njia nyingine ya kutokuwapa watu au vitu nguvu ya kukukwamisha.
Vitu huwa vinakuwa muhimu na vyenye madhara pale tunapovipa uzito.
Kama utaacha kuvipa vitu umuhimu ambao havistahili, haviwezi kukusumbua.
Ukijikagua wewe mwenyewe kwa kuangalia kila eneo la maisha yako, utaweza kuona jinsi ambavyo umekuwa unajikwamisha wewe mwenyewe, kwa kutoa umuhimu mkubwa kwa vitu visivyostahili umuhimu huo.
Kilicho muhimu zaidi kwako ni kupata kile unachotaka.
Unafanya hivyo kwa kupeleka nguvu na umakini wako kwenye njia ambayo inakufikisha kule unakotaka kufika.
Jiruhusu kufanya makubwa na kufikia ndoto zako kubwa kwa kutokutoa nguvu kwa chochote au yeyote kukukwamisha.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani,
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe