Kujipata kwenye maisha yako ni hatua muhimu ambayo hupaswi kuiruka kama unataka kufanikiwa.

Mafanikio hayatokani na juhudi unazoweka pekee, bali yanategemea juhudi hizo unaziweka eneo gani.

Kwa kuweka juhudi kubwa kwenye eneo sahihi, utaweza kupata mafanikio makubwa poa.

Jipate kisha jikite hapo, utafanya makubwa.

Na kama  bado hujajipata, hilo ndiyo linapaswa kuwa kipaumbele cha kwanza kwako.

Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE | +255678977007 | https://bit.ly/makirita