Rafiki,
Kwenye mauzo kuna wakati unaona kabisa mteja wako amevutiwa na bidhaa fulani, lakini ulipomtajia bei unagundua kuwa pesa aliyonayo ni ndogo sana ikilinganishwa na gharama ya bidhaa husika.
Hapa ndipo wauzaji bora na wauzaji wasiobora huonyesha umahiri wao wa kuwasaidia wateja kufanya maamuzi.
Wauzaji bora huwatia moyo wateja wao badala ya kuwakatisha tamaa, wakati huo wauzaji wasio bora huwakatisha tamaa wateja wao.

Katika hali ya namna hiyo wakati wa uhudumiaji unatakiwa kuzingatia yafuatayo;
Moja; Mpe pole kabla hujapendekeza bidhaa nyingine.
Mwambie, “pole sana” Omari au Sara ukweli ni kuwa, bidhaa hii inakufaa sana kulingana na nahitaji yako.
Kwa kuwa umepungukiwa pesa, sina uhakika kama itakufaa, lakini kuna hii bidhaa nyingine nzuri inayofanya kazi kama ile uliyohitaji.
Muonyeshe bidhaa, mweleze kwa kina inayofanya kazi.
Mbili; Mtake alipie pesa iliyopo.
Ikitokea, hajataka kununua bidhaa uliyomuonyesha. Basi unamweleza mteja umuhimu wa kutoondoka na pesa yake. Maana inaweza kutumika nje ya malengo yake.
Analipia kiasi alichonacho, huku akitafuta kiasi kilichobakia. Tunamwambia hivi, ili kukwepa hali ya kurudi nyumbani na pesa yake, ili siku akifanikiwa asiache kuja na kulipia.
Tatu; Mpe matumaini au mchukulie sehemu nyingine
Inawezekana mteja wako kakuta bidhaa imeisha dukani kwako. Ongea naye ukimpa matumaini, “samahani sana, bidhaa uliyotaka imetuishia, lakini tayari tumeshaagiza, na mapema wiki ijayo ukija utaipata, pole sana kwa usumbufu, tafadhali njoo wiki ijayo”
Au Chukua bidhaa sehemu nyingine.
Huenda bidhaa anayohitaji ipo sehemu nyingine au kwa rafiki yako. Hapa unaenda na kuchukua bidhaa na kumpatia mteja wako.
SOMA;Tumia Shukrani Kuwa Muuzaji Bora Na Kufanya Mauzo Makubwa.
Kumbuka, ukimtia moyo na kumpa maneno mazuri mteja wako, unamteka kisaikolojia. Hata kama angeweza kwenda kununua sehemu nyingine, anaweza kusubiri na kurudi tena.

Hatua za kuchukua leo; Kuwa mfariji wa wateja wako badala ya mkatishaji tamaa. Pia, endelea kuwasaidia wateja wako kufanya maamuzi sahihi.
Wako Wa Daima
Lackius Robert
Mkufunzi Msaidizi Chuo Cha Mauzo
0767702659/ mkufunzi@mauzo.tz
Karibu tujifunze zaidi.