Neno shukurani ni dogo sana, lakini lenye maana kubwa kwenye maisha ya binadamu, hasa pale linapotolewa na mtu akalisoma au kulisikia .

Ndiyo maana tunasema, ukitaka kufanikiwa katika mauzo na maisha kwa ujumla kuwa mtu wa shukurani.

Maneno haya, asante na shukurani, yasitoke kinywani mwako. Unajua kwa nini? Shukurani inavuta umakini wa mteja.

Mchakato wa kuwashukuru wateja katika uhudumiaji haupaswi kuwa na ubaguzi wa aina yoyote. Wateja wanaweza kutoa pesa katika viwango tofauti, lakini hawapaswi kubaguliwa.

Maana nne zinazotokana na neno shukurani na asante;

Moja; Kumbukumbu
Unapomshukuru mteja, ina maana unamkumbuka kwa namna alivyofanya siku yako kwenda vema.

Ni watu wengi unaokutana nao, kuongea nao, ulionao kwenye phonebook yako, lakini ni wachache ulioweza kuwatumia ujumbe wa shukurani au uliowashukuru.

Mbili; Kumsifia mteja.
Unapomshukuru mteja, maana yake unamsifu na kumshukuru kufika katika biashara yako au kufanya mawasiliano na wewe.

Mteja hawezi kujishukuru mwenyewe kwa kununua, kuwasiliana au kufika kwako. Unamshukuru wewe. Hivyo, neno àsante sana au nashukuru, linamfanya ajisikie vizuri na ashawishike kupata huduma yako.

Tatu; Kumthamini Mteja
Tunawashukuru watu sio kwa sababu wametupa vitu. Tunawashukuru kwa kutambua thamani yao kwetu.

Iwe umekutana na mteja akanunua au la, mshukuru. Mwambie asante kwa muda wako. Inafanya mtu ajisikie vizuri sana na kuona anathaminiwa.

Nne; Kumuomba aurudi tena.
Unaposhukuru kwa lugha nyepesi; umaanisha kuomba tena.

SOMA; Tumia Kanuni Ya Dakika Mbili Kuushinda Ughairishaji

Ndiyo!
Mteja unayemshukuru, unamtaka arudi tena kununua kwako. Sasa kama ni hivi, kwanini usiwashukuru wateja wengi ili warudi?
Wakati ndio huu!

Muda mzuri wa kuwashukuru wateja ni baada ya mazungumzo, manunuzi au ndani ya masaa 24 za mteja kufika katika huduma yako.

Je, ni wateja wangapi umewashukuru siku ya jana?

Wako Wa Daima

Lackius Robert

Mkufunzi Msaidizi Chuo Cha Mauzo

0767702659/ mkufunzi@mauzo.tz

Karibu Tujifunze Zaidi.