3465; Mshindani atajayekusumbua sana.

Kutoka mezani kwa Kocha,

Rafiki yangu mpendwa,
Hebu fikiria mshindani ambaye anaweza kukusumbua sana kwenye eneo unalopambana kujenga mafanikio makubwa.

Angalia sifa ambazo mshindani akiwa nazo, atakusumbua sana.

Ona jinsi ambavyo mshindani anayeweka umakini wake wote kwenye kile anachofanya anavyokusumbua wewe ambaye unafany mengi.

Unajua jinsi ambavyo ung’ang’anizi huwa unamweka mtu kwenye nafasi nzuri ya kupata anachotaka, kwa sababu hakati tamaa. Ona hilo kwa mshindaji ambaye atakusumbua sana.

Kujifunza endelevu ni moja ya vitu vinavyompa mtu nafasi ya kuwa bora sana na kufanya makubwa. Fikiria mshindani wako ambaye mara zote anajifunza vitu vipya na kufanyia kazi, atakusumbua sana.

Kusema hapana kwa vitu vinavyoonekana ni vizuri lakini havina umuhimu mkubwa ni kitu kinachomwondolea mtu usumbufu unaomkeamisha. Fikiria mshindani ambaye amechagua kile anachofanya na kusema hapana kwa mengine yote.

Rafiki, hizo ni baadhi ya sifa ambazo mshindani akiwa nazo, atakusumbua sana.
Uzuri ni kwamba unazijua kabisa sifa hizo na unaweza kuzijenga kwako mwenyewe.

Sasa una wajibu mkubwa wa wewe kuwa ndiye mshindani unayemhofia zaidi.
Kwa wewe mwenyewe kuwa mshindani wako mkubwa, utaweza kufanya makubwa sana.

Fikiria kila sifa na ubora ambao mshindani akiwa navyo atakusumbua sana, kisha jenga sifa hizo kwako mwenyewe.
Kufanya hivyo kutapelekea wewe kufanya makubwa na kutokuridhika na hatua unazopiga.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr Makirita Amani, MD, CFE.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe