Mitandao ya kijamii ni wavuti au huduma inayotumika kuwaleta watu pamoja kujenga urafiki na kupeana taarifa mbalimbali ikiwemo elimu au biashara

Mitando ya kijamii imekuwa jukwaa muhimu kukutanisha wauzaji na wateja katika zama hizi. Takwimu zilizotolewa October 2023, na mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) zinasema, watumiaji wa intaneti wamefikia milioni.34.4.

Hii kwenye biashara inatoa nafasi ya muuzaji kuwafuatilia na kuwafikia wateja wengi ndani ya muda mchache.

Hii ni kwa sababu watumiaji wengi wanazo simu za smartphone wanazotumia katika kuwasiliana na watu wao wa karibu.

Ndani ya simu hizo ipo mitandao mingi ya kijamii inayokupa nafasi ya kuwafikia kwa ukaribu.

Habari njema kuhusu kufuatilia wateja kitumia mitandao ya kijamii ni kwamba, sio tu unajua biashara zao, bali wao pia, wanaijua biashara yako na kushawishika kununua.

Namna unavyoweza kitumia mitando ya kijamii katika ufuatiliaji wa wateja wako ni pamoja;

Moja; Kulike na kukomenti katika post za Instagram, Facebook, Twitter au LinkedIn.

Mbili; Kutembelea blogu, status, tovutu za wateja wako kuona kile wanachoandika.

Tatu; Kuangalia statu zao na kuwaelekeza namna ya kupost bidhaa zenye mvuto.

Nne; Kupost bidhaa zako au zao na kuwatag katika uwanja wa maoni.

Mitandao ya kijamii ipo mingi, hivyo unapaswa kuchagua mifuko michache ya kufanyia kazi. Ili ufuatiliaji wako uwe na ufanisi.

SOMA; Kufikia Wateja Wengi Kwa Kutumia Maudhui Ya Mitandao Ya Kijamii.

Umuhimu wa kutumia mitando ya kijamii kuwafuatilia wateja wako

Moja; Inasaidia kujenga mahusiano pamoja na kuwafikia wateja wa mbali.

Mbili; Inakuruhusu kuendelea na kazi zako zingine huku ukiendelea na ufuatiliaji wako.

Tatu; Inatambulisha bidhaa zako mbele ya wengine unapotoa maoni au kupost bidhaa, ni rahisi wateja kuona na kuanza kufuatilia biashara yako.

Nne; Inadhibiti idadi ya wateja muhimu katika biashara yako. Hii ni kwa sababu, kama unapost bidhaa zako unawachuja wasiofaa au wasiohitaji huduma yako.

Hatua za kuchukua leo, jua muda sahihi wa kupost bidhaa na wateja wako kuwa “active”. Hii itasaidia ufuatiliaji wako kuwa na ufanisi mkubwa. Usisahau kuandaa bajeti ya kuingia mtandaoni.

Je, ni mtandao upi unatumia kufuatilia wateja wako?

Wako Wa Daima

Lackius Robert

Mkufunzi Msaidizi Chuo Cha Mauzo

0767702659 / mkufunzi@mauzo.tz

Karibu Tujifunze Zaidi.