Utangulizi.

Rafiki yangu mpendwa,

Ninayo furaha kubwa sana ya kukupa taarifa muhimu juu ya tukio ambalo hutokea mara moja kila mwaka.

Hili ni tukio letu la kukutana ana kwa ana watu wote wenye kiu ya mafanikio, ambao wapo ndani ya FAMILIA YA MAFANIKIO ya KISIMA CHA MAARIFA.

Karibu sana kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024, hii ikiwa ni semina ya 9 kufanyika tangu tulipoanza kufanya semina hizi mwaka 2016 bila kukosa hata mwaka mmoja.

Rafiki, SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024 inakwenda kuwa ya tofauti na ya kipekee kabisa ukilinganisha na semina zilizopita.

Makubwa muhimu kuhusu semina hii ni itakuwa ya siku tatu, hivyo kupata nafasi nzuri ya kujifunza kwa kina. Pia itakuwa na gharama nafuu ya ushiriki ambayo kila mtu anaweza kumudu. Na kubwa kuliko yote ni mpango rahisi wa malipo ambao hauwezi kumbana mtu yeyote.

Karibu upate taarifa kamili za semina hapo chini na uchukue hatua mara moja ili usikose nafasi kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024.

Muda, Eneo Na Wanufaika.

SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024 Itafanyika kwa siku 3, kuanzia Ijumaa ya tarehe 25/10/2024 mpaka Jumapili tarehe 27/10/2024. Ni siku tatu za kuondoka na mambo ya kufanyia kazi kwa mwaka mzima.

Semina itafanyika jijini Dar es salaam, kwenye moja ya hoteli ambazo zipo eneo tulivu. Hiyo inatupa nafasi ya kujifunza kwa umakini bila ya usumbufu wowote.

Watu ambao SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024 itawafaa sana na hawapaswi kuikosa ni;

1. Wanaotaka kujenga utajiri na uhuru wa kifedha kwenye maisha yao kwa kuweza kuingiza kipato cha uhakika bila ya kufanya kazi moja kwa moja. Kwenye semina wanakwenda kuondoka na mkakati wa uhakika wa kufanyia kazi na kupata matokeo.

2. Wanaotaka kukuza kipato chao kupitia shughuli wanazofanya, za kuajiriwa na kujiajiri. Hawa wanakwenda kuondoka na njia za kuongeza kipato kwa uhakika.

3. Wanaotaka kukuza mauzo ya biashara zao mara mbili na zaidi ndani ya mwaka mmoja. Hawa watapata mpango wa kutekeleza tu na kupata matokeo.

4. Wanaotaka kumiliki biashara ambazo zinaweza kujiendesha zenyewe bila ya kuwategemea wao moja kwa moja. Hilo linawapa uhuru wa kuanzisha biashara nyingine na kuishi maisha kwa uhuru.

5. Wanaotaka kuwa na usimamizi mzuri wa fedha zao, kuanzia kuongeza kipato, kudhibiti matumizi, kutoka kwenye madeni, kuweka akiba na kufanya uwekezaji. Hawa watatoka wakiwa na mpango kamili wa kutekeleza ili kuwa vizuri kifedha.

Mada Kuu Za Semina.

SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024 itakuwa na mada kuu 4 ambazo washiriki watajifunza kwa kina na kuondoka na hatua za kwenda kutekeleza ili kupata mafanikio.

1. KUJENGA BIASHARA ISIYOKUTEGEMEA.

2. KUKUZA MAUZO MARA MBILI KWA MWAKA.

3. KUISHI MAISHA YA MAFANIKIO.

4. KUWA NA USIMAMIZI MZURI WA FEDHA BINAFSI.

5. KUJENGA UTAJIRI NA KUFIKIA UHURU WA KIFEDHA.

6. KUJIFUNZA KUTOKANA NA MAFANIKIO NA CHANGAMOTO ZA WENGINE.

Vifurushi Na Ada Za Ushiriki.

SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024 itakuwa na vifurushi vya aina tatu ya ushiriki. Vifurushi hivyo vinatoa fursa kwa kila mtu kuweza kushiriki na kuondoka na manufaa makubwa.

A. Kifurushi cha BILIONEA.

1. Kushiriki semina kwa siku tatu, Ijumaa, Jumamosi na Jumapili.

2. Malazi kwa siku zote tatu.

3. Chai ya asubuhi, chakula cha mchana na chakula cha jioni kwa siku zote tatu.

4. Kitabu maalumu, shati na tisheti.

5. Mada kuu ni; KUJENGA BIASHARA ISIYOKUTEGEMEA.

6. Ada ya kushiriki ni Tsh 490,000/= kwa mtu mmoja. Na Tsh 690,000/= ukiwa na mwenza.

7. Nafasi za kifurushi hiki ni 50 pekee.

B. Kifurushi cha MAUZO.

1. Kushiriki semina kwa siku mbili, Jumamosi na Jumapili.

2. Malazi kwa siku zote mbili.

3. Chai ya asubuhi, chakula cha mchana na chakula cha jioni kwa siku zote mbili.

4. Kitabu maalumu, shati na tisheti.

5. Mada kuu ni; KUKUZA MAUZO MARA MBILI KWA MWAKA.

6. Ada ya kushiriki ni Tsh 360,000/= kwa mtu mmoja. Na Tsh 490,000/= ukiwa na mwenza.

7. Nafasi za kifurushi hiki ni 100 pekee.

C. Kifurushi cha UTAJIRI.

1. Kushiriki semina kwa siku moja ambayo ni Jumapili.

2. Chai ya asubuhi na chakula cha mchana kwenye siku ya semina.

3. Mada kuu ni; KUJENGA UTAJIRI NA KUFIKIA UHURU WA KIFEDHA.

4. Ada ya kushiriki ni Tsh 50,000/= kwa mtu mmoja.

5. Nafasi za kifurushi hiki ni 200 pekee.

Kwenye vifurushi vyote unakwenda kupata maarifa bora na sahihi pamoja na mkakati utakaokwenda kufanyia kazi kwa mwaka mzima huku ukifuatiliwa kwa karibu ili kufikia malengo uliyoweka.

Mpango Wa Malipo.

Ili kuhakikisha kwamba kila mtu anapata fursa ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024, kuna mpango maalumu wa malipo ambao ni nafuu kwa kila mtu. Mpango huo ni kama ifuatavyo;

A. Kulipa mara moja.

1. Unalipa ada yote kwa mkupuo mmoja.

2. Kwa kila kifurushi unalipa ada yake kamili, yaani 490,000/= au 360,000/= au 50,000/=

3. Tarehe ya mwisho kulipia ni 30/09/2024

4. Kujihakikishia nafasi, unapaswa kutanguliza Tsh 50,000/= mpaka kufikia tarehe 31/07/2024.

5. Kiasi kilichotangulizwa hakitarudishwa au kubadilishiwa matumizi iwapo mtu hatashiriki semina.

B. Kulipa kila mwezi (awamu 4).

1. Unalipa kwa awamu nne, kila mwisho wa mwezi, kwa miezi ya Julai, Agosti, Septemba na Oktoba 2024.

2. Kwa kifurushi cha BILIONEA unalipa 130,000/=, MAUZO unalipa 95,000/= na UTAJIRI unalipa 14,000/= kila mwezi.

3. Malipo yanaanza mwisho wa mwezi Julai, tarehe ya mwisho kulipia ni 20/10/2024.

4. Kujihakikishia nafasi, unapaswa kulipa awamu ya kwanza mpaka kufikia tarehe 31/07/2024

C. Kulipa kila wiki (awamu 10).

1. Unalipa kwa awamu kumi, kila mwisho wa wiki.

2. Kwa kifurushi cha BILIONEA unalipa 55,000/=, MAUZO unalipa 40,000/= na UTAJIRI unalipa 6,000/= kila mwezi.

3. Malipo yanaanza wiki inayoishia tarehe 14 Julai na kwenda kila wiki mpaka wiki inayoishia tarehe 20 Oktoba 2024.

4. Kujihakikishia nafasi, unapaswa kulipa awamu tatu za mwezi Julai mpaka kufikia tarehe 31/07/2024.

D. Kulipa kila siku (awamu 100).

1. Unalipa kwa awamu mia moja, kila siku.

2. Kwa kifurushi cha BILIONEA unalipa 6,000/=, MAUZO unalipa 4,000/= kila siku na UTAJIRI unalipa 2,000/= kila siku tatu.

3. Malipo yanaanza wiki inayoishia tarehe 8 Julai na kwenda kila siku mpaka tarehe 20 Oktoba 2024.

4. Kujihakikishia nafasi, unapaswa kukamilisha malipo ya awamu zote za mwezi Julai mpaka kufikia tarehe 31/07/2024.

Njia Za Malipo.

Kuhakikisha pia hupati gharama kubwa kwenye kufanya malipo ya ada ya kushiriki semina, tutakuwa na njia mbalimbali za malipo kama ifuatavyo;

1. M-Pesa Lipa Namba: 57774721

Jina: LIPA AMKA CONSULTANTS.

2. NMB Akaunti; 25110031527

Jina: LIPA AMKA CONSULTANTS.

3. CRDB Akaunti; 0152281977700

Jina; Amani Emanuel Makirita

4. M-Pesa; 0752977170

Jina; Amani Emanuel Makirita

5. Tigo Pesa; 0678977007

Jina; Amani Emanuel Makirita

Kwa njia yoyote utakayotumia kulipa, tuma ushahidi kwenda namba 0717396253.

Hatua Ya Kuchukua Sasa.

Ili kujihakikishia kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024, toa taarifa sasa kwa kutuma ujumbe kwenda namba 0717396253.

Kwenye ujumbe andika jina lako na maelezo kwamba utashiriki semina pamoja na kutaja kifurushi cha ushiriki ulichochagua na mpango wako wa malipo.

Mfano wa ujumbe; MIMI AMANI MAKIRITA, NITASHIRIKI SEMINA KWA KIFURUSHI CHA BILIONEA/MAUZO/UTAJIRI. MPANGO WANGU WA MALIPO NI MARA MOJA/ MWEZI/ WIKI/ SIKU.

Baada ya kutuma ujumbe, jiunge kwenye kundi maalumu la wasap la SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza kiungo hiki; https://chat.whatsapp.com/ENw2qEqoO54FrOBXQJsJiq

Hitimisho.

SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024 ni fursa ya kipekee kwa watu wote wenye kiu ya mafanikio kukutana ana kwa ana, kujifunza kwa pamoja na kushirikishana uzoefu wa safari ya mafanikio.

Hii ni fursa ambayo hupaswi kuikosa kabisa, chukua hatua sasa kwa kutuma ujumbe kwenda namba 0717396253 ili ujihakikishie nafasi yako sasa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani,

Medical Doctor (MD) | Certified Financial Educator (CFE).