3482; Yanayotangulia.

Kutoka mezani kwa Kocha,

Rafiki yangu mpendwa,

Mapenzi ya dhati kwenye kitu huwa yanatangulia ung’ang’anizi wa kukifanya kitu hicho.
Na ung’ang’anizi kwenye kile ambacho mtu anafanya huwa unatangulia mafanikio.

Yaani kwa kifupi ni unapenda sana kile unachofanya halafu unakifanya kwa ung’ang’anizi mkubwa kitu kinachokupa mafanikio makubwa.

Inaposisitizwa sana mtu upende kile unachofanya, siyo kwa sababu itakuwa rahisi kufanya. Bali ni kwa sababu utaweza kuendelea kung’ang’ana nacho kwa muda mrefu, hata kama mambo yanakuwa magumu kiasi gani.

Kitu muhimu sana kuhusu mafanikio ni uwezo wa kuendelea kufanya kwa ukubwa na msimamo bila kuacha.
Mtu yeyote anayeweza kupeleka juhudi zake zote kwenye kufanya kitu na akang’ang’ana kwenye kukifanya.

Kwa bahati mbaya sana mapenzi ya dhati juu ya kitu ni kitu ambacho huwezi kufundishwa.
Hicho kinapaswa kuanzia ndani yako mwenyewe.
Lakini bahati nzuri ni kwamba kila mtu kuna vitu ambavyo huwa anavipendelea zaidi.
Mtu akiweza kuvijua na kuvitumia, mafanikio yanakuwa uhakika.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr Makirita Amani,
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe