Rafiki,

Karibu katika mwendelezo wa masomo yetu hapa kwenye program ya Chuo Cha Mauzo yenye kutufanya kuwa wauzaji Bora kuwahi kutokea na kukuza mauzo yetu. 

Leo tutajifunza namna ya kutumia nguvu ya shauku katika utendaji wetu, ili tuwashawishi wateje na kuwauzia wakati wa ufuatiliaji.

Shauku ni kiu,  ni chanzo cha matokeo unayotaka kupata. Hii ni kwa sababu unakuwa na hamasa, imani na kukubali kitu unachofanya.

Kwenye utendaji wako ukifanya kwa shauku unaenda kupata kila kitu unachohitaji kwenye maisha yako.

Ukisoma biblia Mathayo 17;20 inasema, “mkiwa na imani kama punje ya haradali, mtauambia mlima huu ondoka hapa uende pale, nao utaondoka”.

Shauku ni nguvu.
Shauku ni umeme.
Unapokuwa na shauku unavuta nguvu, unaikaribisha attention(umakini )na furaha ya mtu.

Furaha hii hufanya vitu kutokea kwako na wanaokuzunguka. Unapomuona mtu mwenye shauku, moja kwa moja unajawa na nguvu mpya na wewe unaanza kuwa na shauku.

Ukiwa na shauku unaifanya akili yako kuona uwezekano wa vitu. Habari njema kuhusu shauku ni kwamba, huhitaji kuwa na elimu kubwa, bali maamuzi, maana ni zao la ndani yako.

Wataalamu wanasema, shauku sio kujiamini kupitiliza, sio upofu,
ujinga, wala sio utoto, bali ni kupenda unachofanya bila kujali aina ya matokeo unayopata .

Shauku ni kama mziki mzuri unaoupenda kuucheza wakati wote wa maisha yako.

Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Winston Churchill aliwahi kusema, “mafanikio ni kushindwa na kushindwa tena bila kupoteza shauku”.

Mtu mwenye shauku anaambukiza furaha, nguvu kwa watu wa karibu.
Ndiyo maana unasikia watu wakisema, nina furaha kukuona!

Mtu mwenye shauku uambukiza upendo kwa wanaomzunguka. Na utasikia watu wanasema, wow! nimeipenda hii. It’s amazing!

Mtu mwenye shauku hupenda kusaidia wengine. Badala ya kusema fanya peke yako, husema, karibu tufanye kwa pamoja.

Mtu mwenye shauku hutafuta suluhu kwa watu wa karibu. Ndiyo maana, ni rahisi kuleta mabadiliko makubwa kwenye mkutano, mradi, ofisini pamoja na biashara hii kwa sababu ya matokeo makubwa anayozalisha. Mwisho anaweza kubadili maisha yake.

Mambo ya kuzingatia kuwa na shauku kubwa;

Moja; Ongea na moyo wako.
Hii ikiwa na maana kabla hujaongea na mtu yeyote, fanya maongezi ya peke yako, jisikie vile unavyoongea.

Mbili; Jiamini.
Ukijiamini kupitia simu unazopiga matembezi unayofanya na maongezi unayofanya hata wasikilizaji watakuamini na kukupa nafasi.

Tatu; Anza kufanya.
Unapoanza kufanya kitu, ni rahisi kuwa na mwendelezo tofauti na ukiwa hujafanya kitu. Ndiyo maana, kitu kikiwa kwenye mwendo ni rahisi kuendelea.

Nne; Penda na kubali unachofanya.
Ondoa wasiwasi wowote kuhusu aina ya matokeo unayopata. Endelea kufanya kwa msimamo, utapata matokeo makubwa.

SOMA;Ijue Biashara Yako Kwa Kina Ili Ukoe Nguvu Zako

Hivyo, kuwa mwenye shauku mara zote hakika utasikilizwa na kupewa nafasi na wateja wako katika ufuatiliaji unaofanya na watakupa kile unachotaka.

Wako Wa Daima Lackius Robert

Mkufunzi Msaidizi Chuo Cha Mauzo

0767702659/ mkufunzi@mauzo.tz

Karibu tujifunze zaidi.