Habari njema wauzaji bora kuwahi kutokea.

Karibu katika mwendelezo wa masomo yetu ya programu ya CHUO CHA MAUZO yenye lengo la kutujenga kuwa wauzaji bora kuwahi kutokea na kukuza mauzo yetu.

Leo tutajifunza namna ya kupata wateja bora au  wazuri na kuwashawishi kununua tena.

Ipo wazi kuwa, kila biashara kuna wateja ambao ipo nao, bila kujali imeanza kuuza lini.

Wateja hao ambao biashara inao inaweza kuwatumia kuongeza mauzo zaidi ya mara mbili.

Kama muuzaji bora kuwahi kutokea hii ni nafasi yako kuchagua wateja wazuri kutoka kwenye orodha uliyonao na kuwashawishi kununua zaidi.

Katika hili kuna hatua muhimu za kuzingatia ili kupata wateja wazuri;

Hatua ya kwanza; Fanyia tathimini wateja waliopo.
Hii ifanyike kwa kuangalia manunuzi ya mteja kuanzia kiwango cha juu hadi chini. Ikiwa na maana ya mteja anayefanya manunuzi makubwa hadi madogo. Hii ni muhimu kwa sababu inakusaidia kujua mteja yupi umpe nguvu na umakini.

Tunafahamu wateja ni wahongo. Kwenye mauzo usiamini maneno ya mteja, amini mifuko yao baada ya kutoa pesa.

Hatua ya pili; Jifanyie tathimini juu ya wateja unaowapenda na unaowachukia.
Kwenye biashara zetu, kuna wateja ambao tunawauzia basi tu, lakini wanatusumbua sana. Kwa kuwa tunataka pesa yao, tunawahudumia, ila sio kwamba tunawapenda.

Vile vile kuna wengine tunawaopenda sana. Hawa ni wepesi kusikiliza ushauri, kupokea simu ata kufanya manunuzi.

Unapofanya tathimini unagundua wateja unaowapenda ni rahisi kuwahudumia haraka kuliko unaowachukia.

Kwa Kufanya hivyo, unajua wapi uongeze jitihada katika kuwa karibu na wateja, japo hata unaowachukia ni wateja wa kumshawishi kuuzia

Hatua ya tatu; Ainisha jamii waliyomo.
Kila mteja ana jamii yake ambapo ni rahisi kumpata. Mfano mzuri wa jamii ni kama ilivyo jamii ya Kisima Cha Maarifa.

Unakuwa ni mkusanyiko wa watu wenye nia moja ya kufanikiwa au kupiga hatua. Ukiwa katika jamii hiyo ni rahisi kumpata mteja akakupa ushirikiano mzuri.

Hatua ya nne; Ainisha maeneo wanayopenda kwenda (kupumzika).
Hapa unaangalia maeneo ambayo wanapendelea kuwa. Hii inasaidia katika kulainisha mawasiliano,  maana mnakuwa na point za kugusia na kuongeza ushawishi.

Baada ya hapo andaa chati ya wateja hata kumi unaowapenda na unaowachukia. Ainisha jamii waliyomo na maeneo wanayopenda kwenda kimatembezi au kupumzika. Kisha endelea kuwa nao karibu kiasi kwamba hawawezi kununua sehemu nyingine.

Hatua za kuchukua leo; Jua vema aina ya wateja wako, wapi unaowapenda zaidi, wapi unaowachukia. Kisha endelea kuwashawishi na kuwauzia.

SOMA; Tumia mitando ya kijamii kuwafuatilia wateja

Wakati wako ndio huu.

Wako Wa Daima Lackius Robert

Mkufunzi Msaidizi Chuo Cha Mauzo

0767702659/ mkufunzi@mauzo.tz

Karibu tujifunze zaidi.