3522; Ona vitu jinsi vilivyo.

Kutoka mezani kwa Kocha,

Rafiki yangu mpendwa,

Kinachowakwamisha watu kwenye maisha ni kushindwa kuona vitu jinsi vilivyo, kwa uhalisia wake.

Watu huwa wanaona kile wanachotaka kuona na kusikia wanachotaka kusikia.
Matokeo yake ni kutokuujua ukweli, kitu ambacho kinawakwamisha kwenye mambo mengi.

Hilo huanzia kwenye utoto na ujana na baadaye kuwa tabia iliyokomaa.
Ikishakomaa kama tabia, huwa inakuwa ngumu kuvunja.
Hapo ndipo maisha ya wengi huishia na kukwama kufanya makubwa kwenye maisha yao.

Kila ambapo mtu anapanga na kujaribu makubwa, anaishia kupata matokeo ambayo siyo mazuri.
Hiyo ni kwa sababu haendi na ukweli, bali anaenda na mazoea.

Kuondokana na hilo jisukume kutoka nje ya mazoea yoyote uliyonayo.
Kwa kila unachopanga na kufanya, jiulize ni namna gani unaweza kufanya tofauti na ulivyozoea.
Kila mara jilazimishe kuona vitu tofauti na jinsi ulivyozoea.

Pia kwa kila unachofanya, mwisho jitathmini.
Unajitathmini yale uliyofanya na matokeo uliyopata.
Kisha unaangalia ni kwa namna gani unaweza kuboresha yale unayofanya ili kupata matokeo bora zaidi.

Kufanya hivyo unajilazimisha kuona vitu kwa jinsi vilivyo kiuhalisia.
Hilo linakuwezesha kufanya maamuzi bora yanayotokana na mtu kuutafuta ukweli.

Kadiri unavyoendelea kwenda, pambana sana kuvunja mazoea ambayo yamekuwa yanakukwamisha kufanya makubwa.
Jijengee utaratibu ambao unakulazimisha kuona vitu kwa uhalisia wake na kufanya maamuzi sahihi kwenye mambo yako yote.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE
+255 678 977 007 | http://www.amkamtanzania.com

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe