3524; Kipimo rahisi cha nafasi na fedha.
Kutoka mezani kwa Kocha,
Rafiki yangu mpendwa,
Kupima kwa haraka mafanikio ambayo mtu anaweza kujenga angalia ukubwa wa mambo yanayomsumbua.
Kama mtu anasumbuliwa na mambo madogo madogo, ni dhahiri kwamba hawezi kujenga mafanikio makubwa.
Kama mtu hawezi kuwa na uvumilivu pale anapopitia changamoto za aina fulani, hawezi kuvuka changamoto kubwa atakazokabiliana nazo kwenye mafanikio makubwa.
Kama mtu anakimbia magumu na kukimbilia mambo rahisi kufanya, hawezi kujenga mafanikio makubwa na yanayodumu, maana hayo ni magumu zaidi.
Kama mtu anakata tamaa haraka pale anapokutana na vikwazo, hakuna namna ataweza kujenga mafanikio makubwa, maana hayo yana vikwazo vya kila aina.
Unaweza kuvumilia msongo na usumbufu kiasi gani ndiyo itaamua kiwango cha mafanikio unayoweza kupata.
Usijione mjanja kukimbilia mambo rahisi, jua unajizuia kupata mafanikio makubwa ambayo yangeweza kubadili kabisa maisha yako.
Jipime wewe mwenyewe kwenye maeneo hayo, kukabiliana na msongo, usumbufu, ugumu na kushindwa uone uko imara kiasi gani.
Jiimarishe kwenye maeneo hayo ili uweze kufanya makubwa na kufanikiwa sana kwenye maisha yako.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE
+255 678 977 007 | http://www.amkamtanzania.com
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe