3526; Utateseka sana mpaka utakapokubali hili.

Kutoka mezani kwa Kocha,

Rafiki yangu mpendwa,

Kwenye biashara na ujasiriamali, watu wamekuwa wanateseka sana kwa sababu moja tu; hawapo tayari kufanya ambacho hawapendi kufanya.

Wakati mafanikio kwenye kila eneo la maisha yanataka mtu uwe tayari kufanya yale usiyopenda kufanya.
Maana hayo ndiyo wengine pia hawapendi kuyafanya.
Na kwa kuwa wengi hawapendi kuyafanya, thamani yake inakuwa kubwa.

Tukirudi kwenye biashara na ujasiriamali, watu wapo tayari kuweka fedha zao walizotafuta kwa jasho kwenye biashara.
Wapo tayari kwenda mbali zaidi na kukopa fedha ambazo watalipa kwa gharama.

Watakazana kuandaa bidhaa au huduma wanazouza.
Halafu watakaa kusubiri wateja waje.
Na wateja hawaji.
Wanaishia kulalamika kwamba biashara ni ngumu.

Biashara inakuwaje ngumu wakati hakuna hata watu ambao umewakera?
Unataka uonekane mstaarabu siyo, hutaki kuwa msumbufu kwa watu.
Na ndiyo maana utateseka sana.

Kama hutaki kuteseka kwenye biashara na ujasiriamali, PIGA KELELE SANA.
Yaani PIGA KELELEEEEE.
Sauti haijatosha, PIGA KELELEEEEEE

Kama siku inapita na hakuna watu uliowakera kwa kuitangaza biashara yako, huitangazi vya kutosha.

Najua utasema ukipiga kelele sana, ukiwasumbua watu, watachukia na kuacha kununua.
Na mimi nakuambia kama mteja amekataa kununua kwa sababu unapiga kelele sana, asingenunua hata usingepiga kelele.
Hivyo PIGA KELELEEEEE.

Wateja sahihi watafurahia kelele zako, watanunua hata kama hawataki, kwa kuheshimu kelele zako.

Na watakaokataa kununua kwa sababu ya kelele zako, watakutangaza vizuri sana.
Kwa hiyo piga KELELEEEE.

Unaogopa kupiga kelele ni bangi unauza?
Hebu PIGA KELELEEEE.

Unaweza kuwa na bidhaa bora sana.
Unaweza kuwa na huduma ya kipekee kabisa.
Lakini kama hutapenda sana kupiga kelele,
Utaishia kulalamika mambo ni magumu.
PIGA KELELEEE…
Ndiyo namna pekee ya kutoboa kwenye biashara na ujasiriamali.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE
+255 678 977 007 | http://www.amkamtanzania.com

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe