3530; Hakikisha unashinda.
Kutoka mezani kwa Kocha,
Rafiki yangu mpendwa,
Watu wamekuwa wepesi sana kwenye kutaka ushindi.
Wanapokutana na changamoto au vikwazo vya kawaida, wanaacha kupambania walichotaka.
Hiyo imepelekea watu wengi kuanza mambo na kuishia njiani.
Kama unataka ushindi, unapaswa tu kuhakikisha unashinda.
Fanya kila unachopaswa kufanya ili kujihakikishia ushindi.
Na njia za kujihakikishia hilo ni mbili; KUJIFUNZA na KAZI.
Unapaswa kujifunza na kujua kile unachofanya kuliko mwingine yeyote. Hakikisha kwa namna unavyojua, wengine wanajiona wazi kwamba hakuna wanachojua.
Na endelea kujua kwa kasi kiasi cha ambao wangetaka kukusumbua, inawabidi wajifunze kwako.
Kuwa kipimo cha kujifunza kwenye tasnia uliyopo, yaani watu wanapojifunza, wanalinganisha wamefikia hatua gani kwa kukuangalia wewe.
Halafu sasa inakuja kwenye kazi. Unapaswa kufanya kazi kwa juhudi kubwa kuliko wengine wote.
Unapaswa kuweka muda mwingi kwenye kazi, kwa umakini mkubwa sana.
Unapaswa kufanya kazi kiasi cha wengine kuwafanya wengine watilie mashaka maisha yao.
Wafanye watu wajione kama vile wanacheza tu, hakuna wanachofanya kila wakijilinganisha na wewe.
Huhitaji hata kujua watu wanafanya kazi kwa juhudi kiasi gani, unachopaswa kuhakikisha ni haiwezekani kibinadamu mtu mwingine akawa anafanya kama wewe.
Nenda kabisa nje ya mazoea yote ambayo watu wanayo ili uweze kufanya makubwa sana.
Kama kwa kujifunza hapa umeona hiyo siyo kwa ajili yako, upo sahihi kabisa.
Kubali maisha ya kawaida na sindikiza wengine hapa duniani.
Lakini kama hutaki kuwa msindikizaji, basi hakikisha uwepo wako unawakosesha watu amani, kwa jinsi unavyofanya mambo yako.
Kama inabidi ufanye kazi mara 10 zaidi ya wengine ndiyo upate ushindi, hicho ndiyo unachopaswa kufanya. Fanya.
Usitake makuu, huku pia ukitaka uwe kawaida. Fanya yale unayopaswa kufanya, ili tu kuhakikisha unapata ushindi unaoutaka.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE
+255 678 977 007 | www.amkamtanzania.com
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe