3531; Je ndiyo bora zaidi?
Kutoka mezani kwa Kocha,
Rafiki yangu mpendwa,
Watu huwa wanaanzia chini kabisa, wanapambana sana na kufikia ngazi fulani ya mafanikio.
Lakini baada ya kufika ngazi hiyo ya mafanikio, wanakuwa hawaendelei tena kupiga hatua.
Wanaganda hapo na kuanza kuanguka.
Hilo limekuwa linasababishwa na tabia ya watu kuridhika haraka na kuacha kujiuliza swali hili muhimu; Je hii ndiyo bora zaidi?
Kwa kila unachokuwa nacho, hilo ndiyo swali unalopaswa kujiuliza bila kukoma.
Kwa hatua unayokuwa umefikia, jiulize je hiyo ndiyo hatua bora zaidi kuliko zote?
Kwa kipato unachokuwa unaingiza, jiulize je hicho ndiyo kipato cha juu kabisa unachoweza kuingiza?
Hata kwa watu unaokuwa nao, unapaswa kujiuliza je hao ndiyo watu bora kabisa unaoweza kuwa nao?
Hilo ni swali rahisi ambalo ukijiuliza na kujipa maswali sahihi, huwezi kuridhika na chochote unachokuwa nacho au unachokuwa umepata.
Kila wakati unapaswa kutafuta kilicho bora zaidi ya kile ulichonacho.
Unapaswa kupambana kwenda zaidi ya pale ulipo.
Ni msukumo huo ndiyo utakaokuwezesha kufanya makubwa zaidi kwenye maisha yako.
Pale unapojikuta unashawishika kumpa mtu kazi kwa sababu ni ndugu yako, jiulize kama huyo ndiyo mtu bora zaidi kwenye kazi hiyo anayepatikana hapa duniani.
Kama jibu ni hapana, jua umeridhika haraka na hutaweza kupata matokeo makubwa.
Kila mara pambana kupata kilicho bora zaidi na utajenga mafanikio endelevu wakati wote.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE
+255 678 977 007 | www.amkamtanzania.com
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe