Rafiki yangu mpendwa,
Najua umeshashiriki semina nyingi sana, ambazo zilikupa matumaini makubwa ya kubadili maisha yako, lakini bado umebaki pale ulipokuwa.
Najua umesoma vitabu ambavyo vilikuahidi kupata siri za mafanikio na utajiri, ukapata hamasa baada ya kusoma, lakini ni muda umekwenda na bado uko hapa.
Hayo yanaweza kuwa yamekupelekea ukose imani kwenye maarifa na mafunzo mbalimbali ambayo yamekuwa yanatolewa.
Na upo sahihi kabisa, kwamba mafunzo mengi yanayotolewa, yamekuwa hayaleti mabadiliko kwenye maisha ya wengi.
Lakini leo nina habari njema sana kwako, habari za mafunzo ya kipekee ambayo ukiyapata utakwenda kupindua kabisa meza kwa upande wako wa kifedha.

Mafunzo hayo ni SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024 ambayo taarifa zake ziko hapo chini. Pitia kwa makini kisha chukua hatua mara moja.
Karibu Kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024.
Semina hii inakwenda kukupa maarifa sahihi ya KUPATA, KUTUNZA na KUZALISHA fedha kwa kutumia nguzo saba unazopaswa kuzijua.
Nguzo hizo saba za kukuwezesha kuwa imara kifedha ni kama ifuatavyo;
1. KIPATO; Kikubwa, Uhakika na Endelevu.
2. AKIBA; Dharura, Malengo na Nidhamu.
3. MATUMIZI; Mahitaji, Matakwa na Anasa.
4. MADENI; Mazuri, Mabaya na Kutokomeza.
5. MATOLEO; Sadaka, Misaada na Kodi.
6. UWEKEZAJI; Masoko, Hatifungani na Mali.
7. ULINZI (BIMA); Afya, Mali na Maisha
Kwenye nguzo hizo saba unakwenda kujifunza kwa vitendo na kutoka na hatua za kwenda kuchukua ili uwe imara kifedha.
Hupaswi kukosa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024 kama upo makini na fedha zako.
Semina itafanyika Mbezi Garden Hotel DSM tarehe 27/10/2024.
Ada ya kushiriki semina ni Tsh 65,000/= Kama utalipa kabla ya tarehe 01/10/2024 na kuanzia tarehe 01/10/2024 ada ya kushiriki itakuwa Tsh 100,000/=.
Kushiriki piga simu au tuma ujumbe wa kawaida au kwa wasap kwenda namba 0752977175 wenye maneno SEMINA 2024 na utapewa utaratibu mzima na nafasi ya kushiriki.
Karibu rafiki uchukue hatua sasa ili kufanya uwekezaji bora kabisa kwako, utakaoacha alama kubwa kifedha kwako.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi