Rafiki yangu mpendwa,
Umekuwa unakaa kinyonge kwenye fedha, kwa sababu umekuwa hujiamini. Ukiwa huna fedha ni matatizo, kwa sababu unakuwa hujui kwa uhakika unazipata wapi.
Lakini pia ukiwa na fedha ni matatizo, kwa sababu unakuwa unashindwa kuzitumia kwa usahihi, hivyo kuishia kuzipoteza zote.
Ni jambo la kushangaza sana kwamba eneo la fedha linakutesa pande zote. Ukiwa nazo unateseka na usipokuwa nazo pia unateseka.
Yote hayo yanatokana na ukweli kwamba hatukupata nafasi ya kupewa elimu sahihi inapokuja kwenye fedha.
Yote tunayojua na kufanya kuhusu fedha, tunabahatisha tu. Tunaiga wengine wanavyofanya, ambao nao hawakupata nafasi ya kujifunza popote.
Yaani ni kama vipofu ambao wanaongozana na mwisho wake ni kuanguka kwenye shimo linalowapoteza kabisa.
Kwenye fedha mashimo hayo ni matumizi kuwa makubwa kuliko mapato, kuwa na madeni mabaya na kukosa ulinzi wa kifedha.

Rafiki, habari njema ni kwamba kuna fursa nzuri kwako ya kutokukaa tena kinyonge inapokuja kwenye swala la fedha. Kwa kuchukua hatua kwenye fursa hiyo, utaondoka kwenye mashimo yote ya kifedha ambayo umeshaingia mpaka sasa.
Fursa hiyo itakayokutoa kwenye unyonge wa kifedha ni SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024 ambayo taarifa zake ziko hapo chini. Pitia kwa makini kisha chukua hatua mara moja.
Karibu Kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024.
Semina hii inakwenda kukupa maarifa sahihi ya KUPATA, KUTUNZA na KUZALISHA fedha kwa kutumia nguzo saba unazopaswa kuzijua.
Nguzo hizo saba za kukuwezesha kuwa imara kifedha ni kama ifuatavyo;
1. KIPATO; Kikubwa, Uhakika na Endelevu.
2. AKIBA; Dharura, Malengo na Nidhamu.
3. MATUMIZI; Mahitaji, Matakwa na Anasa.
4. MADENI; Mazuri, Mabaya na Kutokomeza.
5. MATOLEO; Sadaka, Misaada na Kodi.
6. UWEKEZAJI; Masoko, Hatifungani na Mali.
7. ULINZI (BIMA); Afya, Mali na Maisha
Kwenye nguzo hizo saba unakwenda kujifunza kwa vitendo na kutoka na hatua za kwenda kuchukua ili uwe imara kifedha.

Hupaswi kukosa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024 kama upo makini na fedha zako.
Semina itafanyika Mbezi Garden Hotel DSM tarehe 27/10/2024.
Ada ya kushiriki semina ni Tsh 65,000/= Kama utalipa kabla ya tarehe 01/10/2024 na kuanzia tarehe 01/10/2024 ada ya kushiriki itakuwa Tsh 100,000/=.
Kushiriki piga simu au tuma ujumbe wa kawaida au kwa wasap kwenda namba 0752977175 wenye maneno SEMINA 2024 na utapewa utaratibu mzima na nafasi ya kushiriki.
Karibu rafiki uchukue hatua sasa ili kufanya uwekezaji bora kabisa kwako, utakaoacha alama kubwa kifedha kwako.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi