Rafiki yangu mpendwa,
Kwenye kundi la FAMILIA YA MAFANIKIO YA KISIMA CHA MAARIFA, mmoja wa wanachama ameshirikisha picha ya SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA iliyofanyika mwaka 2019 na kusema; “Lilikuwa tukio kubwa sana !!”
Huo ni ukweli ulio wazi, kwa sababu SEMINA ZA KISIMA CHA MAARIFA ambazo zimekuwa zinafanyika kila mwaka tangu mwaka 2016, zimekuwa zinaleta mapinduzi makubwa kwa wote wanaoshiriki.

Kila anayeshiriki semina hizi, siyo tu anajifunza kutoka kwenye masomo yaliyoandaliwa, lakini pia anajifunza kutoka kwa washiriki wengine. Na asikuambie mtu, hakuna kitu kinawasukuma watu kama kuona wengine wameweza kupiga hatua fulani ambazo wao bado hawajapiga.
Nilipoona ujumbe wa mshiriki huyu wa nyuma, nikakumbuka jinsi ambavyo maandalizi ya semina ya mwaka huu yalivyo makubwa. Ninachotaka kukuambia na kukuhakikishia ni kwamba, SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024 inakwenda kuwa kubwa kuliko zote.
Linakwenda kuwa tukio kubwa sana, ambalo litaacha alama kubwa kwenye maisha yako. Unakwenda kupata mapinduzi makubwa sana kwenye eneo la fedha.
Utaondoka kwenye semina hii ukiwa na hatua za uhakika za kuchukua ili kuleta matokeo ya tofauti kwenye maisha yako.
Na hata baada ya semina, hutabaki kinyonge, bali kutakuwa na ufuatiliaji wa kuhakikisha kweli unayafanyia kazi uliyojifunza.
Hayo na mengine mengi, unakwenda kuyapata kwenye semina ya mwaka huu. Taarifa zaidi ziko hapo chini.
Karibu Kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024.
Semina hii inakwenda kukupa maarifa sahihi ya KUPATA, KUTUNZA na KUZALISHA fedha kwa kutumia nguzo saba unazopaswa kuzijua.
Nguzo hizo saba za kukuwezesha kuwa imara kifedha ni kama ifuatavyo;
1. KIPATO; Kikubwa, Uhakika na Endelevu.
2. AKIBA; Dharura, Malengo na Nidhamu.
3. MATUMIZI; Mahitaji, Matakwa na Anasa.
4. MADENI; Mazuri, Mabaya na Kutokomeza.
5. MATOLEO; Sadaka, Misaada na Kodi.
6. UWEKEZAJI; Masoko, Hatifungani na Mali.
7. ULINZI (BIMA); Afya, Mali na Maisha
Kwenye nguzo hizo saba unakwenda kujifunza kwa vitendo na kutoka na hatua za kwenda kuchukua ili uwe imara kifedha.
Hupaswi kukosa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024 kama upo makini na fedha zako.
Semina itafanyika Mbezi Garden Hotel DSM tarehe 27/10/2024.
Ada ya kushiriki semina ni Tsh 65,000/= Kama utalipa kabla ya tarehe 01/10/2024 na kuanzia tarehe 01/10/2024 ada ya kushiriki itakuwa Tsh 100,000/=.
Kushiriki piga simu au tuma ujumbe wa kawaida au kwa wasap kwenda namba 0752977175 wenye maneno SEMINA 2024 na utapewa utaratibu mzima na nafasi ya kushiriki.
Karibu rafiki uchukue hatua sasa ili kufanya uwekezaji bora kabisa kwako, utakaoacha alama kubwa kifedha kwako.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi
