Rafiki yangu mpendwa,

Ulipokuwa mtoto, wazazi wako walikuonya usicheze na watoto fulani kwa sababu ya tabia zao. Hukupenda kabisa kukatazwa hilo, lakini baadaye umekuja kuona matokeo yake kwenye maisha.

Kama tayari ni mzazi au mlezi, unawaonya watoto wasicheze na watoto wenye tabia za aina fulani. Kwa sababu unajua jinsi ambavyo tabia zinaambukizwa kirahisi.

Swali ninalotaka kukuliza ni je unajua madhara ya tabia za watu wanaokuzunguka sasa, ukiwa mtu mzima? Kwa sababu kile unachowaonya watoto, ndiyo unachohitaji wewe.

Wale wanaokuzunguka, ambao unatumia nao muda wako mwingi wanaathiri sana tabia zako. Uko hivyo ulivyo sasa kutokana na mchango wa wanaokuzunguka.

Kama unataka kubadili maisha yako, anza kwa kubadili watu wanaokuzunguka. Kwa bahati mbaya sana, huenda ulipo huna watu sahihi wa kuambatana nao ili kufanikiwa.

Hilo siyo tatizo tena, kwani kuna jukwaa sahihi kwako kuwapata watu sahihi watakaokusukuma ufanikiwe.

Kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024 unakwenda kupata fursa ya kukutana na watu sahihi watakaokusukuma ufanikiwe.

Karibu ushiriki semina hii ili uzungukwe na watu sahihi watakaokuchochea ufanikiwe.

Karibu Kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024.

Semina hii inakwenda kukupa maarifa sahihi ya KUPATA, KUTUNZA na KUZALISHA fedha kwa kutumia nguzo saba unazopaswa kuzijua.

Nguzo hizo saba za kukuwezesha kuwa imara kifedha ni kama ifuatavyo;

1. KIPATO; Kikubwa, Uhakika na Endelevu.

2. AKIBA; Dharura, Malengo na Nidhamu.

3. MATUMIZI; Mahitaji, Matakwa na Anasa.

4. MADENI; Mazuri, Mabaya na Kutokomeza.

5. MATOLEO; Sadaka, Misaada na Kodi.

6. UWEKEZAJI; Masoko, Hatifungani na Mali.

7. ULINZI (BIMA); Afya, Mali na Maisha

Kwenye nguzo hizo saba unakwenda kujifunza kwa vitendo na kutoka na hatua za kwenda kuchukua ili uwe imara kifedha.

Hupaswi kukosa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024 kama upo makini na fedha zako.

Semina itafanyika Mbezi Garden Hotel DSM tarehe 27/10/2024.

Ada ya kushiriki semina ni Tsh 65,000/= Kama utalipa kabla ya tarehe 01/10/2024 na kuanzia tarehe 01/10/2024 ada ya kushiriki itakuwa Tsh 100,000/=.

Kushiriki piga simu au tuma ujumbe wa kawaida au kwa wasap kwenda namba 0752977175 wenye maneno SEMINA 2024 na utapewa utaratibu mzima na nafasi ya kushiriki.

Karibu rafiki uchukue hatua sasa ili kufanya uwekezaji bora kabisa kwako, utakaoacha alama kubwa kifedha kwako.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi