3541; Mpaka lini utaendelea kulipia kukumbushwa hili?
Kutoka mezani kwa Kocha,
Rafiki yangu mpendwa,
Hakuna kitu ambacho kimewapoteza wengi kama kutafuta njia ya mkato ya mafanikio.
Kila wakati huwa zipo njia za mkato zinazouzwa kwa ushawishi mkubwa sana.
Na kwa sababu watu wana tamaa kubwa ya kufanikiwa, huwa wanaishia kulizwa.
Wanaingia gharama kubwa na wanaishia kupata funzo kwamba hakuna njia ya mkato ya mafanikio.
Lakini bado hawachoki, akitokea mtu mwingine anayeahidi mafanikio ya haraka bila kazi, wanajiambia safari hii ni tofauti.
Wanaingia na wanaliwa tena.
Hivi ndivyo watu wanavyoenda kwa miaka mingi, wakihangaika sana lakini wasifanikiwe.
Wakati wangetumia muda huo huo, kujenga mafanikio yao kwa njia ndefu, wangefanikiwa kwa uhakika.
Ambacho mtu unapaswa kufanya ili upate mafanikio makubwa kinaeleweka wazi kabisa.
Jua thamani unayotoa kwa wengine, iwe ni kwenye ajira, kujiajiri au biashara.
Lazima uanze kwa kuwapa wengine thamani.
Piga kelele sana kuhakikisha wengi wanajua thamani unayotoa. Hakikisha wote wanaoweza kunufaika na kile unachotoa, wanajua kuhusu uwepo wako na jinsi wanavyoweza kunufaika.
Wapende sana wale wanaokulipa kupata thamani unayotoa. Wape kipaumbele cha kwanza, wafanye wanufaike kuliko hata walivyotarajia.
Endelea kutoa thamani kubwa zaidi na endelea kupiga kelele kuwafikia wengi zaidi.
Weka kichwa chako chini kwenye huo mchakato bila ya mahangaiko mengine na mafanikio yatakuwa yako, kwa uhakika.
Au utaendelea kulipa gharama kubwa, kwa fedha, nguvu na muda, kukumbushwa kwamba hakuna njia ya mkato.
Umeamua nini?
Utadumuje kwenye hayo maamuzi?
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE
+255 678 977 007 | http://www.amkamtanzania.com
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe