Rafiki yangu mpendwa,

Umekuwa unapata mafunzo ya aina mbalimbali ambayo yamekuwa yanakupa hamasa kubwa ya kuchukua hatua ya kuyabadili maisha yako.

Huenda ni kushiriki semina ambayo mafunzo uliyopata yalikupa hamasa kubwa sana. Au ni kitabu ambacho umesoma na kikakuonyesha jinsi unaweza kufanya makubwa.

Unaanza kutekeleza yale uliyojifunza, ukiona jinsi ambavyo yanakwenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.

Lakini kwa bahati mbaya sana, hizo huishia kuwa mbio za panya, au nguvu za soda. Kwani umekuwa haudumu na hilo kwa muda mrefu. Unajikuta umeacha na kurudi kwenye mazoea yako.

Kama umechoshwa na hilo na ungetaka kubadili hali hiyo, kama unataka uweze kuyafanyia kazi yale unayojifunza na kunufaika nayo, kuna nafasi nzuri na yenye manufaa kwako.

Nafasi hiyo ni kushiriki kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024, ambapo hutajifunza tu kwa nadharia, bali kwa vitendo. Semina hii itakuwa tofauti kabisa na nyingine ulizoshiriki kwa sababu utaondoka na mambo ya kwenda kufanyia kazi moja kwa moja.

Karibu sana ushiriki semina hii na uweze kuleta mabadiliko ya kweli kwenye maisha yako.

Karibu Kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024.

Semina hii inakwenda kukupa maarifa sahihi ya KUPATA, KUTUNZA na KUZALISHA fedha kwa kutumia nguzo saba unazopaswa kuzijua.

Nguzo hizo saba za kukuwezesha kuwa imara kifedha ni kama ifuatavyo;

1. KIPATO; Kikubwa, Uhakika na Endelevu.

2. AKIBA; Dharura, Malengo na Nidhamu.

3. MATUMIZI; Mahitaji, Matakwa na Anasa.

4. MADENI; Mazuri, Mabaya na Kutokomeza.

5. MATOLEO; Sadaka, Misaada na Kodi.

6. UWEKEZAJI; Masoko, Hatifungani na Mali.

7. ULINZI (BIMA); Afya, Mali na Maisha

Kwenye nguzo hizo saba unakwenda kujifunza kwa vitendo na kutoka na hatua za kwenda kuchukua ili uwe imara kifedha.

Hupaswi kukosa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024 kama upo makini na fedha zako.

Semina itafanyika Mbezi Garden Hotel DSM tarehe 27/10/2024.

Ada ya kushiriki semina ni Tsh 65,000/= Kama utalipa kabla ya tarehe 01/10/2024 na kuanzia tarehe 01/10/2024 ada ya kushiriki itakuwa Tsh 100,000/=.

Kushiriki piga simu au tuma ujumbe wa kawaida au kwa wasap kwenda namba 0752977175 wenye maneno SEMINA 2024 na utapewa utaratibu mzima na nafasi ya kushiriki.

Karibu rafiki uchukue hatua sasa ili kufanya uwekezaji bora kabisa kwako, utakaoacha alama kubwa kifedha kwako.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi