Rafiki yangu mpendwa,
Tatizo kubwa sana la fedha siyo sisi wenyewe pekee, bali hata wale wanaotuzunguka wamekuwa wanachangia.
Kwenye jamii zetu, ukiweza kupambana na ukawa na kipato kikubwa kuliko wengine, unageuka kuwa tegemeo kwao wote.
Na hakuna ubaya kuwa tegemeo kwa watu wa karibu, lakini mategemeo ya wengi yanakuwa siyo sahihi.
Watu wako wa karibu wanakuwa wanaamini kwa sababu wewe una fedha, basi una wajibu wa kuwapa fedha.
Wewe unaweza kukazana kuwasaidia ili nao waweze kupata fedha kama wewe, lakini wao hawatathamini hilo, watakachotaka ni uwape fedha.
Na usipowapa fedha, wanakuona wewe ni mbaya na usiyejali kuhusu watu wako wa karibu.
Hiyo ni hali ambayo inakusumbua sana, na wakati mwingine kujisikia vibaya kwa kuwa na fedha kuliko wanaokuzunguka.

Rafiki, nina habari njema kwako za jinsi ya kukabiliana na hilo. Kwa watu wako wa karibu ambao wamekuwa hawakuelewi kwenye eneo la fedha, njoo nao kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024.
Kwa kushiriki semina hiyo na watu wako wa karibu, watajifunza misingi yote muhimu ya fedha na watapunguza utegemezi wa kutaka wewe uwape fedha. Badala yake wataweza kujijenga vizuri kifedha na kuwa huru.
Huwa kuna kauli inasema usiwape watu samaki, bali wafundishe kuvua. Kwenye fedha, usiwape watu fedha, bali njoo nao kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2024 wapate elimu sahihi ya fedha.
Karibu Kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024.
Semina hii inakwenda kukupa maarifa sahihi ya KUPATA, KUTUNZA na KUZALISHA fedha kwa kutumia nguzo saba unazopaswa kuzijua.
Nguzo hizo saba za kukuwezesha kuwa imara kifedha ni kama ifuatavyo;
1. KIPATO; Kikubwa, Uhakika na Endelevu.
2. AKIBA; Dharura, Malengo na Nidhamu.
3. MATUMIZI; Mahitaji, Matakwa na Anasa.
4. MADENI; Mazuri, Mabaya na Kutokomeza.
5. MATOLEO; Sadaka, Misaada na Kodi.
6. UWEKEZAJI; Masoko, Hatifungani na Mali.
7. ULINZI (BIMA); Afya, Mali na Maisha
Kwenye nguzo hizo saba unakwenda kujifunza kwa vitendo na kutoka na hatua za kwenda kuchukua ili uwe imara kifedha.
Hupaswi kukosa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024 kama upo makini na fedha zako.
Semina itafanyika Mbezi Garden Hotel DSM tarehe 27/10/2024.
Ada ya kushiriki semina ni Tsh 65,000/= Kama utalipa kabla ya tarehe 01/10/2024 na kuanzia tarehe 01/10/2024 ada ya kushiriki itakuwa Tsh 100,000/=.
Kushiriki piga simu au tuma ujumbe wa kawaida au kwa wasap kwenda namba 0752977175 wenye maneno SEMINA 2024 na utapewa utaratibu mzima na nafasi ya kushiriki.
Karibu rafiki uchukue hatua sasa ili kufanya uwekezaji bora kabisa kwako, utakaoacha alama kubwa kifedha kwako.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi