Rafiki yangu mpendwa,

Inapokuja kwenye swala la fedha, kumekuwa na imani nyingi ambazo zimekuwa zinawaathiri sana watu. Imani hizo, iwe ni sahihi au siyo, kitendo cha mtu kuzikubali kinakuwa na athari.

Moja ya imani hizo ni ‘chuma ulete’, dhana kwamba kuna watu wenye nguvu ya kuchukua fedha za watu bila wao kujua. Hivyo wengi wanapopata fedha lakini hawajui zinaishia wapi, wanalaumu uwepo wa chuma ulete ambao wanawaibia fedha hizo.

Ni kweli kama ‘chuma ulete’ yupo, ndiyo maana huzioni fedha zako. Lakini chuma ulete mwenyewe siye unayemdhania. Kama umeanza kufikiria baadhi ya watu kuwa ndiyo wamesababisha wewe upoteze fedha bila kujua, umejichanganya.

Chuma ulete anayekusumbua wewe ni matumizi ambayo umekuwa unafanya nje ya bajeti yako. Ukiwa huna fedha, unakuwa na mawazo mazuri, lakini ukizipata, zinaisha bila kutekeleza mawazo hayo.

Yote ni kwa sababu ya matumizi yanayojitokeza nje ya bajeti uliyokuwa nayo, kama hata una bajeti. Unaishia kujikuta fedha zimeisha na bado una mahitaji ya fedha.

Rafiki, nina habari njema kwako za jinsi ya kukabiliana na chuma ulete huyo ambaye amekuwa anakukwamisha sana. Kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024 unakwenda kujifunza namna bora ya kudhibiti matumizi yako kwa kuwa na bajeti sahihi na unayoifuata.

Karibu Kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024.

Semina hii inakwenda kukupa maarifa sahihi ya KUPATA, KUTUNZA na KUZALISHA fedha kwa kutumia nguzo saba unazopaswa kuzijua.

Nguzo hizo saba za kukuwezesha kuwa imara kifedha ni kama ifuatavyo;

1. KIPATO; Kikubwa, Uhakika na Endelevu.

2. AKIBA; Dharura, Malengo na Nidhamu.

3. MATUMIZI; Mahitaji, Matakwa na Anasa.

4. MADENI; Mazuri, Mabaya na Kutokomeza.

5. MATOLEO; Sadaka, Misaada na Kodi.

6. UWEKEZAJI; Masoko, Hatifungani na Mali.

7. ULINZI (BIMA); Afya, Mali na Maisha

Kwenye nguzo hizo saba unakwenda kujifunza kwa vitendo na kutoka na hatua za kwenda kuchukua ili uwe imara kifedha.

Hupaswi kukosa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024 kama upo makini na fedha zako.

Semina itafanyika Mbezi Garden Hotel DSM tarehe 27/10/2024.

Ada ya kushiriki semina ni Tsh 65,000/= Kama utalipa kabla ya tarehe 01/10/2024 na kuanzia tarehe 01/10/2024 ada ya kushiriki itakuwa Tsh 100,000/=.

Kushiriki piga simu au tuma ujumbe wa kawaida au kwa wasap kwenda namba 0752977175 wenye maneno SEMINA 2024 na utapewa utaratibu mzima na nafasi ya kushiriki.

Karibu rafiki uchukue hatua sasa ili kufanya uwekezaji bora kabisa kwako, utakaoacha alama kubwa kifedha kwako.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi