Rafiki yangu mpendwa,

Watu wengi wanapokuwa wanaanzia chini na hawana fedha, huwa wanadhani tatizo pekee la fedha walilonazo ni kuzikosa.

Hali hiyo inawasukuma kupambana sana ili kutoka kwenye hali hiyo ya kukosa fedha. Na baadhi wanafanikiwa kutoka kwenye hiyo hali.

Lakini kitu kinachokuja kuwashangaza ni jinsi ambavyo matatizo yao ya fedha hayaishi licha ya kuwa nazo.

Badala yake tatizo linabadilika kutoka kukosa fedha mpaka kuwa na fedha. Yaani mtu alikuwa ana tatizo la kukosa fedha halafu anapozipata na zenyewe zinakuwa tatizo pia.

Rafiki, ukweli ni kwamba, inapokuja kwenye fedha huwa kuna matatizo mawili; moja ni kutokuwa na fedha na mbili ni kuwa na fedha.

Kama unataka kuwa vizuri kwenye eneo la fedha, ni lazima uyajue matatizo yote mawili ya fedha na namna bora ya kuyakabili.

Tatizo la kukosa fedha utalitatua kwa kuweka juhudi kubwa kuingiza kipato. Lakini je unajua tatizo la kuwa na fedha unalitatuaje?

Unajua nini unapaswa kufanya pale unapokuwa na kipato cha kutosheleza mahitaji yako na kuzidi? Huenda unadhani ni swali rahisi, lakini angalia watu wengi waliopambana na kuweza kutoka kwenye umasikini, lakini baadaye wakaanguka na kurudi kwenye umasikini mkubwa.

Hicho ndiyo kitu ambacho sitaki kitokee kwako wewe rafiki yangu. Ndiyo maana nimekuandalia fursa nzuri kwako kujifunza tatizo la pili la fedha ili lisiwe kikwazo kwako.

Karibu Kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024.

Semina hii inakwenda kukupa maarifa sahihi ya KUPATA, KUTUNZA na KUZALISHA fedha kwa kutumia nguzo saba unazopaswa kuzijua.

Nguzo hizo saba za kukuwezesha kuwa imara kifedha ni kama ifuatavyo;

1. KIPATO; Kikubwa, Uhakika na Endelevu.

2. AKIBA; Dharura, Malengo na Nidhamu.

3. MATUMIZI; Mahitaji, Matakwa na Anasa.

4. MADENI; Mazuri, Mabaya na Kutokomeza.

5. MATOLEO; Sadaka, Misaada na Kodi.

6. UWEKEZAJI; Masoko, Hatifungani na Mali.

7. ULINZI (BIMA); Afya, Mali na Maisha

Kwenye nguzo hizo saba unakwenda kujifunza kwa vitendo na kutoka na hatua za kwenda kuchukua ili uwe imara kifedha.

Hupaswi kukosa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024 kama upo makini na fedha zako.

Semina itafanyika Mbezi Garden Hotel DSM tarehe 27/10/2024.

Ada ya kushiriki semina ni Tsh 65,000/= Kama utalipa kabla ya tarehe 01/10/2024 na kuanzia tarehe 01/10/2024 ada ya kushiriki itakuwa Tsh 100,000/=.

Kushiriki piga simu au tuma ujumbe wa kawaida au kwa wasap kwenda namba 0752977175 wenye maneno SEMINA 2024 na utapewa utaratibu mzima na nafasi ya kushiriki.

Karibu rafiki uchukue hatua sasa ili kufanya uwekezaji bora kabisa kwako, utakaoacha alama kubwa kifedha kwako.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi