Rafiki yangu mpendwa,
Huwa kuna nauli inayosema; ‘Mungu akitaka kumwadhibu mtu, huwa anampa kile anachokitaka sana.’
Tumekuwa tunaona uhalisia wa kauli hiyo kwenye maisha yetu na ya watu wengine. Pale tunapokuwa tunakitaka kitu sana na kupambana kila namna kukipata, huwa tunaamini tukishakipata ndiyo jawabu la kila kitu.
Lakini cha kushangaza, tunapokipata kitu hicho, haturidhiki kwa jinsi ambavyo tulitegemea. Unakuta tuliachana na mengine mengi ili kupambania kitu hicho. Lakini baada ya kukipata tunajiuliza; ‘Ni hiki tu? Hakuna kingine zaidi?’
Tunakuwa tulianza na matarajio makubwa sana na kudhani matokeo tutakayopata yatamaliza kila kitu. Lakini kwenye uhalisia hilo linakuwa tofauti. Na hicho ndiyo chanzo cha watu wengi kukosa furaha, licha ya kupata kila wanachotaka.

Kwenye fedha hili ni kubwa na lenye madhara zaidi. Ukiwa huna fedha unapambana ukiamini ukipata fedha basi maisha yako yatakuwa raha na starehe milele. Ni mpaka unapopata fedha zaidi ya unavyotaka na bado maisha yako hayawi ya raha na starehe.
Kwa sehemu kubwa, kupata fedha nyingi kama unavyotaka ni adhabu ambayo itakutesa sana. Hiyo ni kwa sababu kwa kukosa maandalizi sahihi, wengi huishia kuteswa na fedha wanazopata kuliko kunufaika.
Rafiki, simaanishi usipate fedha, pata nyingi sana, lakini hakikisha una maandalizi sahihi ili ukwepe adhabu kali inayokuja na fedha.
Na maandalizi hayo sahihi yanapatikana kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024.
Karibu Kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024.
Semina hii inakwenda kukupa maarifa sahihi ya KUPATA, KUTUNZA na KUZALISHA fedha kwa kutumia nguzo saba unazopaswa kuzijua.
Nguzo hizo saba za kukuwezesha kuwa imara kifedha ni kama ifuatavyo;
1. KIPATO; Kikubwa, Uhakika na Endelevu.
2. AKIBA; Dharura, Malengo na Nidhamu.
3. MATUMIZI; Mahitaji, Matakwa na Anasa.
4. MADENI; Mazuri, Mabaya na Kutokomeza.
5. MATOLEO; Sadaka, Misaada na Kodi.
6. UWEKEZAJI; Masoko, Hatifungani na Mali.
7. ULINZI (BIMA); Afya, Mali na Maisha
Kwenye nguzo hizo saba unakwenda kujifunza kwa vitendo na kutoka na hatua za kwenda kuchukua ili uwe imara kifedha.
Hupaswi kukosa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024 kama upo makini na fedha zako.
Semina itafanyika Mbezi Garden Hotel DSM tarehe 27/10/2024.
Ada ya kushiriki semina ni Tsh 65,000/= Kama utalipa kabla ya tarehe 01/10/2024 na kuanzia tarehe 01/10/2024 ada ya kushiriki itakuwa Tsh 100,000/=.
Kushiriki piga simu au tuma ujumbe wa kawaida au kwa wasap kwenda namba 0752977175 wenye maneno SEMINA 2024 na utapewa utaratibu mzima na nafasi ya kushiriki.
Karibu rafiki uchukue hatua sasa ili kufanya uwekezaji bora kabisa kwako, utakaoacha alama kubwa kifedha kwako.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi