Rafiki yangu mpendwa,
Inapokuja kwenye fedha, watu wamehangaishwa na mambo mengi ambayo yamekuwa hayafanyi kazi.
Kumekuwa na njia nyingi za mkato zinazowaahidi watu utajiri wa haraka tena bila ya kufanya kazi. Lakini mara zote njia hizo zimekuwa zinaishia kuwagharimu watu na kuishia kupoteza fedha zao.
Wale ambao wameshaumizwa na hizo njia za mkato wamekosa kabisa imani kwamba wanaweza kujenga utajiri mkubwa. Huku ambao bado hawajaumizwa wakiendelea kutafuta njia za aina hiyo.
Rafiki, habari njema nilizonazo ni kwamba ipo njia sahihi ya kukuwezesha wewe kugeuza shilingi elfu 1 kuwa shilingi bilioni 1. Njia hiyo haihusishi miujiza au utapeli wa aina yoyote.

Njia ya kufanya hivyo ni kupitia uwekezaji wa muda mrefu, kwa msimamo bila kuacha. Mtu yeyote anayeweza kufanya uwekezaji wa shilingi elfu moja kila siku, ambayo ni sawa na elfu 30 kwa mwezi, akawekeza eneo linalompa marejesho ya 12%, hivi ndivyo ukuaji wa uwekezaji wake utakavyokwenda;
Mwaka 1 inakuwa Tsh 380,475.09
Miaka 5 inakuwa Tsh 2,450,090.10
Miaka 10 inakuwa Tsh 6,901,160.68
Miaka 20 inakuwa Tsh 29,677,660.96
Miaka 30 inakuwa Tsh 104,848,923.98
Miaka 40 inakuwa Tsh 352,943,175.31
Miaka 50 inakuwa Tsh 1,171,750,191.00
(NB; Ukokotoaji huu umefanyika kwa kutumia kikokotoo cha UTT AMIS kinachopatikana hapa; https://uttamis.co.tz/tools/monthly-calculator Kiasi cha kuwekezwa kila mwezi kimewekwa 30,000/= na riba ya 12% kwa mwaka ambao ndiyo wastani wa marejesho kwa mifuko ya UTT AMIS).
Rafiki, hizo siyo ndoto za alinacha, bali ni uhalisia kabisa. Na kama ungependa kupata mkakati kamili wa kutekeleza hilo, karibu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024.
Karibu Kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024.
Semina hii inakwenda kukupa maarifa sahihi ya KUPATA, KUTUNZA na KUZALISHA fedha kwa kutumia nguzo saba unazopaswa kuzijua.
Nguzo hizo saba za kukuwezesha kuwa imara kifedha ni kama ifuatavyo;
1. KIPATO; Kikubwa, Uhakika na Endelevu.
2. AKIBA; Dharura, Malengo na Nidhamu.
3. MATUMIZI; Mahitaji, Matakwa na Anasa.
4. MADENI; Mazuri, Mabaya na Kutokomeza.
5. MATOLEO; Sadaka, Misaada na Kodi.
6. UWEKEZAJI; Masoko, Hatifungani na Mali.
7. ULINZI (BIMA); Afya, Mali na Maisha
Kwenye nguzo hizo saba unakwenda kujifunza kwa vitendo na kutoka na hatua za kwenda kuchukua ili uwe imara kifedha.
Hupaswi kukosa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024 kama upo makini na fedha zako.
Semina itafanyika Mbezi Garden Hotel DSM tarehe 27/10/2024.
Ada ya kushiriki semina ni Tsh 65,000/= Kama utalipa kabla ya tarehe 01/10/2024 na kuanzia tarehe 01/10/2024 ada ya kushiriki itakuwa Tsh 100,000/=.
Kushiriki piga simu au tuma ujumbe wa kawaida au kwa wasap kwenda namba 0752977175 wenye maneno SEMINA 2024 na utapewa utaratibu mzima na nafasi ya kushiriki.
Karibu rafiki uchukue hatua sasa ili kufanya uwekezaji bora kabisa kwako, utakaoacha alama kubwa kifedha kwako.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi