Mahafali ya kuhitimu mafunzo ama elimu yoyote ni wakati wa furaha sana kwa wahitimu. Furaha hiyo inatokana na kukamilisha na kupata ujuzi mtu aliokuwa anasomea ama kujifunza. Katika furaha hiyo hiyo kuna wengi wanafurahia kwa sababu ndio wamemaliza kusoma hivyo hawatajisomea tena mpaka labda watakapokuja kuendeea ngazi ya juu ya eimu hiyo. Tumekuwa tukisikia watu wakitoa kauli za kwamba shue imeisha hivyo wanaachana na kusoma na kuanza kufanya mambo yao.
Watanzania hatuna sana mwamko wa kujisomea vitabu mbalimbali. Ndio maana hata shuleni na vyuoni wengi hujisomea kwa sababu tu kuna mtihani na usipojisomea utafeli mtihani na hutofuzu mafunzo yako. Hii ndio inafanya mtu kufurahia kumaliza mafunzo kwa sababu unaona ndio umeachana na vitabu.
Kama una mpango wa kuachana na vitabu baada ya masomo ama ulishaachana na vitabu ulipomaliza masomo basi jua upo katika njia mbovu ambayo inaelekea kukupoteza. Kwenye ulimwengu wa sasa ambao mambo yanabadiika kwa kasi ni rahisi sana kuachwa nyuma kama hakuna kipya unachoingiza kwenye kichwa chako kia siku. Hizi ni zama za taarifa ambapo wenye taarifa sahihi ndio wanaotawala.
Ili kupata taarifa na kungeza ufahamu wako ni vyema ukapenda kujisomea. Weka utaratibu wa kujisomea vitabu ambavyo vinahusiana na kile unachofanya ama kile unachopendelea. Kwa kujisomea vitabu utapata maarifa na mbinu mbalimbali zitakazokufanya uwe na ujuzi zaidi na uwe umebobea kwenye hicho unachofanya.
Sina muda wa kujismea kila siku, niko ‘bize’ sana.
Unaweza ukawa umeshaelewa umuhimu wa kujisomea ila tatizo lako ni moja tu, huna muda. Ni kwei kabisa unaweza kuwa huna muda kutokana na mihangaiko ya sasa na ugumu wa maisha, lakini hupaswi kukosa muda mfupi wa kujisomea kila siku. Tenga japo nusu saa tu kwa siku ya kujisomea, hakuna unaloweza kupoteza kwa kutenga nusu sasa(tena kwa kuwahi kuamka asubuhi) kila siku. Bonyeza hapa kwa kupata mpango mzuri wa muda wa kujisomea.
Sina vitabu vya kujisomea.
Inawezekana unapenda sana kujisomea ama umeshaona umuhimu wa kujisomea, na umeshaweka ratiba nzuri ya kujisomea kila siku ila huna vitabu vya kujisomea. Kwa uimwengu wa sasa vitabu vinapatikana kiurahisi mno, licha ya vitabu pia kuna mitandao mingi inayotoa taarifa nzuri za wewe kuweza kujiendeleza. Kama unataka kitabu chochote cha kada yoyote unayofanya ama unayopendelea unaweza kuwasiliana na mimi na nikakupatia kitabu unachotaka bila gharama yoyote. Bonyeza hapa na utapata mawasiiano yangu ya email au namba ya simu.
Kama hujawa na utaratibu wa kujisomea vitabu mpaka sasa hujachelewa kama utaamua kuchukua hatua leo. Jiwekee ratiba ya kusoma vitabu na ndani ya muda mfupi utaanza kuona matunda yake kwa lolote unalofanya.