3552; Hakuna kingine muhimu zaidi.

Kutoka mezani kwa Kocha,

Rafiki yangu mpendwa,

Kama ingekuwa kutaka mafanikio ndiyo kufanikiwa kwenyewe, kila mtu angekuwa tayari ana mafanikio makubwa.

Lakini kwenye uhalisia, kuyataka mafanikio na kuyapata ni vitu viwili tofauti kabisa.

Kila mtu anayataka mafanikio.
Lakini siyo kila mtu yupo tayari kuweka juhudi zinazohitajika ili kuyapata mafanikio hayo.
Na ni wachache sana walio tayari kuvumilia magumu yaliyopo kwenye safari ya mafanikio.

Na kilicho kigumu zaidi kufanya kwenye safari ya mafanikio ni kuzikataa fursa ambazo ni nzuri, ili kufanyia kazi kwa uhakika fursa moja bora uliyochagua.

Unafanikiwa kwa uhakika pale unapochagua kitu kimoja na kukipa umakini wako wote.
Hicho ndiyo kinakuwa kitu muhimu zaidi kuliko vingine vyote.

Umakini na fikra zako zote zinakuwa kwenye hicho muhimu na kupuuza vitu vingine vyote.

Ni nguvu ya umakini uliokusanya kwenye kitu kimoja ndiyo inayoleta matokeo makubwa na ya kipekee, ambayo hayajawahi kupatikana kwa namna nyingine.

Unafanikiwa kwa uhakika pale unapochagua kitu kimoja kinachokuwa muhimu zaidi kuliko vingine vyote.
Kisha unakipa kitu hicho umakini na juhudi zako zote mpaka kupata matokeo unayoyataka.

Rafiki, ni kitu gani kimoja ambacho umechagua kukipa umakini na juhudi zako zote kiasi cha kutoruhusu usumbufu mwingine wowote? Hapo ndipo unapoweza kuyajenga mafanikio makubwa unayoyataka.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE
+255 678 977 007 | http://www.amkamtanzania.com

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe