Rafiki yangu mpendwa,

Nimekuwa nakupata taarifa za tukio kubwa la mafanikio linalotokea mara moja tu kwa mwaka. Tukio hilo ni SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024, ambapo unapata nafasi ya kujifunza na kukutana na wengine ambao mnafanana kwenye mtazamo wa mafanikio.

Kwa mwaka huu 2024 tukio hilo linafanyika tarehe 27/10/2024 Mbezi Garden Hotel Dar es salaam.

Taarifa muhimu ninayotaka kukupa leo rafiki ni kuhusu gharama za kushiriki tukio hili muhimu. Tumeweka gharama za msingi kabisa ambazo zinalipa mahitaji ya siku nzima ya mafunzo.

Kwa sababu mafunzo ya semina ni ya siku nzima, kuanzia asubuhi mpaka jioni, kunakuwa na chai ya asubuhi, chakula cha mchana na vifaa vya kujifunzia. Vyote hivyo vina gharama.

Ada ya kushiriki semina ni Tsh 65,000/= ambayo yote inaenda kwenye hizo gharama. Nafasi ya kulipa ada hiyo ni mpaka kufikia tarehe 30/09/2024. Kuanzia tarehe 01/10/2024 ada ya kushiriki itakuwa Tsh 100,000/= ambayo ndiyo ada halisi ambayo ingepaswa kutozwa.

Hapa nakupa taarifa kwamba zimebaki siku 7 pekee kupata nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024 kwa gharama nafuu kwako. Chukua hatua sasa ili usikose nafasi hii ya kipekee.

Karibu Kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024.

Semina hii inakwenda kukupa maarifa sahihi ya KUPATA, KUTUNZA na KUZALISHA fedha kwa kutumia nguzo saba unazopaswa kuzijua.

Nguzo hizo saba za kukuwezesha kuwa imara kifedha ni kama ifuatavyo;

1. KIPATO; Kikubwa, Uhakika na Endelevu.

2. AKIBA; Dharura, Malengo na Nidhamu.

3. MATUMIZI; Mahitaji, Matakwa na Anasa.

4. MADENI; Mazuri, Mabaya na Kutokomeza.

5. MATOLEO; Sadaka, Misaada na Kodi.

6. UWEKEZAJI; Masoko, Hatifungani na Mali.

7. ULINZI (BIMA); Afya, Mali na Maisha

Kwenye nguzo hizo saba unakwenda kujifunza kwa vitendo na kutoka na hatua za kwenda kuchukua ili uwe imara kifedha.

Hupaswi kukosa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024 kama upo makini na fedha zako.

Semina itafanyika Mbezi Garden Hotel DSM tarehe 27/10/2024.

Ada ya kushiriki semina ni Tsh 65,000/= Kama utalipa kabla ya tarehe 01/10/2024 na kuanzia tarehe 01/10/2024 ada ya kushiriki itakuwa Tsh 100,000/=.

Kushiriki piga simu au tuma ujumbe wa kawaida au kwa wasap kwenda namba 0752977175 wenye maneno SEMINA 2024 na utapewa utaratibu mzima na nafasi ya kushiriki.

Karibu rafiki uchukue hatua sasa ili kufanya uwekezaji bora kabisa kwako, utakaoacha alama kubwa kifedha kwako.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi